Dereva huyo, Chrispin Inyangwe (40) alipigwa risasi ya mgongoni alipojaribu kupambana nao.
Tukio
hilo lilitokea usiku wa kuamkia jana eneo la katikati ya vijiji vya
Miula na Kalundi vilivyopo Kata ya Kipande wilayani Nkasi.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Rukwa, George Kyando alisema wafanyabiashara hao
walikuwa wakitokea mnadani na walipofika eneo hilo walikuta mawe
yamepangwa barabarani kuzuia magari.
Alisema
baada ya kuona mawe hayo, magari hayo yalilazimika kusimama na ndipo
majambazi hao waliokuwa na silaha za moto, mapanga na marungu
walipoibuka na kufyatua risasi hewani na baadaye kutaka wafanyabiashara
hao wasalimishe fedha na simu zao za mkononi.
Kamanda huyo alisema baadhi ya wafanyabiashara walisalimisha fedha na simu zao, na waliokataa walishambuliwa.
Inasemekana
kwamba Inyangwe ambaye alikuwa dereva wa gari aina ya Mitsubishi Canter
alikaidi kutoa fedha na kutaka kupambana nao, ndipo watu hao waliokuwa
na bunduki aina ya SMG walipomfyatulia risasi iliyompata mgongoni na
kufariki dunia papo hapo.
Kitendo
hicho kiliwafanya wafanyabiashara wengine waliokuwa wakikataa kutoa
fedha, kuzisalimisha sambamba na simu zao, ndipo majambazi hao
walipowaachia na kukimbia.
Watu
19 waliojeruhiwa walipelekwa Hospitali ya Mkoa mjini Sumbawanga.
Kamanda Kyando alisema majeruhi 12 waliruhusiwa kurejea nyumbani na
wengine saba wanaendelea na matibabu na kwamba polisi wanaeendelea na
msako wa watu hao.
0 comments:
Post a Comment