Waziri mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa amehitimisha mkutano wa nne wa bunge la kumi na moja bungeni Dodoma ambapo katika hotuba yake aliongelea hali ya kiuchumi ya nchi baada ya baadhi ya taarifa za wasiwasi wa kiuchumi kudondoka zikiwa zimetawala.
‘Hivi karibuni kumekuwa na wasiwasi kuhusu mwenendo wa kiuchumi hususani kifedha, napenda kuwahakikishia watanzania kuwa mwenendo wa uchumi ni wakuridhisha na unaendelea kuimarika‘ –Waziri mkuu Majaliwa
‘Mabank yetu yapo salama na yana mitaji ya kutosha, wizara ya fedha na bank kuu ya Tanzania vinafuatilia kwa ukaribu kuhusu mwenendo wa hali ya uchumi nchini‘ –Waziri mkuu Majaliwa
‘Hali ya uchumi ni shwari kabisa na si kama inavyozaniwa na baadhi ya watu, katika taarifa ya bank kuu imebainisha kuwa katika robo ya mwaka 2016 ukuaji wa uchumi umeendelea kuwa wa kuridhisha kwa kuwa na ukuaji wa asilimia 5.5 ukilinganisha na asilimia 5.7 kipindi cha mwaka 2015‘
–Waziri mkuu Majaliwa
0 comments:
Post a Comment