Showing posts with label Hot. Show all posts
Showing posts with label Hot. Show all posts

DEREVA Bodaboda Aliyembeba Mmiliki wa Nyoka wa Ajabu Afunguka A-Z (Video)

Tukio lililozua taharuki kwa wakazi wa Songea mkoani Ruvuma na kupewa nafasi kubwa katika vyombo vya habari vya Tanzania na nje ya Tanzania pamoja na mitandao ya kijamii, huku likiacha gumzo midomoni mwa watu, kuhusiana na kifo cha Denis Komba kufariki dunia baada ya nyoka wake aliyekuwa anasadikiwa kummiliki, kuuawa na wananchi DESEMBA 26.

Ruvuma TV imezungumza na KASIANI HAULE, ambaye ndiye dereva boda boda aliyekuwa kakodiwa na marehemu DENISI KOMBA Bonyeza hiyo Video upate ukweli wa tukio.

MAKUBWA Yafichuka Faru John

Maofi sa wa Wizara ya Maliasili na Utalii, wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA), wafanyakazi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) na maofi sa Taasisi ya Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) wakiwamo madaktari, wakifanya uchunguzi wa Faru John baada ya kufa katika eneo la Sasakwa Grumeti.


SAKATA la kutoweka kwa faru John lililoibuliwa wakati wa ziara ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa katika mikoa ya Arusha na Manyara linazidi kuchukua sura mpya kila kukicha.

Taarifa zilizolifikia MTANZANIA baada ya kufanya uchunguzi wa sakata hilo kwa wiki kadhaa sasa, zinaonyesha kwamba uamuzi wa kumhamisha faru huyo kutoka Hifadhi ya Bonde la Ngorongoro ulihusisha mamlaka za kitaifa za Serikali.

Habari kutoka vyanzo vya kuaminika zinaeleza kwamba mchakato wa kuhamishwa kwa faru John kutoka Hifadhi ya Bonde la Ngorongoro kwenda Grumeti, ulianza katika eneo la Nyasirori ndani ya Hifadhi ya Serengeti Aprili 17, 2015.

Uamuzi huo kwa mujibu wa vyanzo vya uhakika serikalini, ulianza siku hiyo hiyo wakati wa tukio la kuwafungulia mbwa mwitu waliokuwa wamehifadhiwa katika eneo maalumu huko Nyasirori.

Vyanzo vya uhakika vya habari vinaeleza kwamba mjadala kuhusu kuhamishwa kwa faru John ulifanyika wakati watendaji wakuu wa taasisi za uhifadhi za Serikali zinazounda Kamati Maalumu ya Kuwalinda Tembo na Faru (National Elephant and Rhino Steering Committee) wakiwapo.

Miongoni mwa watendaji wanaotajwa kuwapo wakati wa mjadala kuhusu kuhamishwa kwa faru huyo kutoka katika Bonde la Ngorongoro kutokana na sababu za kitaalamu, ni Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka ya Bonde la Ngorongoro (NCAA), Dk. Fadhili Manongi na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), Allan Kijazi.

Wengine ni Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti ya Wanyamapori (TAWIRI), Dk. Simon Mduma na mwakilishi wa Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori aliyefahamika kwa jina la Alex Choya.

Taarifa kuhusu kuwapo kwa haja ya kuhamishwa kwa faru huyo zilipelekwa hadi Wizara ya Maliasili na Utalii.

Kufikishwa kwa suala hilo wizarani kulifuatiwa na hatua ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dk. Adelhem Meru, kuwaandikia barua watendaji wa Mamlaka ya Bonde la Ngorongoro kutekeleza uamuzi huo ifikapo Desemba 31, 2015.

Alipoulizwa kuhusu uwapo wa barua hiyo, Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe, alisema ni kweli barua hiyo ipo kwenye kumbukumbu za wizara.

“Ni kweli hiyo document ipo, lakini hili suala la faru John linafanyiwa kazi na vyombo vya dola. Nadhani si vizuri kulijadili kwa undani sasa, tusubiri matokeo ya uchunguzi,” alisema Waziri Maghembe.

Wahifadhi kadhaa waliozungumza na gazeti hili kutoka Serengeti na Ngorongoro juu ya sakata hilo, walieleza kwamba kiini cha kufikiwa kwa uamuzi huo kulitokana na mabadiliko makubwa ya kitabia aliyokuwa nayo faru John tangu mwaka 2002.

“Faru John alizaliwa ndani ya Ngorongoro, na alianza kuonyesha tabia za ukorofi dhidi ya faru wengine madume mwaka 2002,” alieleza mhifadhi mmoja anayefanya kazi Ngorongoro.

Mhifadhi mwingine alimweleza mwandishi wetu kwamba hali hiyo ilisababisha Mamlaka ya Bonde la Ngorongoro kufanya mawasiliano na TAWIRI kuhusu hatua za kuchukua.

Alisema kuwa hali ilizidi kuwa mbaya na mwaka 2005 kiliitishwa kikao kingine kujadili matatizo ya faru John ambaye tabia yake ya kuwapiga faru wengine ilisababisha wanyama hao kutoka ndani ya Ngorongoro na hivyo kusababisha ugumu wa kuwalinda.

“Tatizo jingine lililotokana na ubabe wa faru John, ni gharama kubwa za ulinzi wa faru waliokimbia vipigo, na kutawanyika hadi kwenye mashamba ya watu.

“Faru wana tabia moja, pindi wanapopigana, yule aliyeshindwa huondoka eneo husika,” alieleza mhifadhi mwingine aliyezungumza na MTANZANIA.

Taarifa kutoka Ngorongoro zinaeleza kuwa mwaka 2013 tatizo la faru John lilizidi kuwa baya zaidi pale kreta, baada ya faru huyo kuua wenzake wawili.

Katika tukio hilo, faru John anatajwa aliua ndama (jike) kwa kumchoma na pembe na kisha akaua dume mwenzake katika mapigano.

Mhifadhi huyo aliliambia gazeti hili kwamba faru John ndiye aliyekuwa na watoto wengi katika Bonde la Ngorongoro kuliko faru mwingine yeyote.

Tukio la faru John kumuua ndama kwa pembe lilitokea wakati alipokuwa akijaribu kumpanda mama yake.

“Faru John alianza kuwapanda watoto wake, jambo ambalo kitaalamu si salama kwa uhai wa faru, hivyo kuendelea kumwacha pale kreta lilikuwa jambo la hatari.

“Baada ya matukio hayo ya 2013, kikao kilikaa tena ambapo TANAPA pia walihudhuria, swali kubwa likiwa ni wapi ambako faru John alipaswa kupelekwa?” alisema mhifadhi mwingine.

Kwa mhifadhi huyo, uamuzi wa kwanza ulikuwa ni kumtoa faru John na kumpeleka katika Hifadhi ya Mkomazi ambako kuna makazi maalumu ya faru (rhino sanctuary).

Hifadhi ya Mkomazi ambako hata hivyo uamuzi huo ulikwama, iko chini ya uendeshaji wa mwekezaji Tony Fitz John.

Kukwama kwa uamuzi huo wa kwanza pia kunaelezwa kulisababishwa na taarifa kwamba katika Hifadhi ya Mkomazi kulikuwa na uwiano sawa kati ya faru madume na majike.

Taarifa nyingine zinasema mwaka huo huo wa 2013, ulifikiwa uamuzi mwingine wa kumkata pembe faru huyo kama njia ya kupunguza madhara aliyokuwa akisababisha katika hifadhi, jambo ambalo lilifanyika.

Wakati wahifadhi wakiumiza vichwa kuhusu nini kifanyike, faru wawili waliokuwa Grumeti, waitwao Limpopo (dume) na Laikipya (jike) walipoteza maisha.

Taarifa zinasema Limpopo aliuawa wakati akipigana na tembo, wakati sababu za kifo cha Laikipya hazikutajwa.

Upungufu huo wa faru wawili ndiyo sababu ambayo baadaye ilisababisha kuzaliwa kwa hoja ya faru John kupelekwa Grumeti kupanda na kuzalisha majike.

Hali hiyo inatajwa kuwa ndiyo iliyosababisha uongozi wa Grumeti inayomilikiwa na tajiri wa Marekani, Paul Tudo Jones, waandike barua ya kuomba faru dume kwa Mkurugenzi wa Wanyamapori, jambo ambalo lilifanyika.

Vyanzo vya habari kutoka serikalini vinaeleza kuwa baada ya maombi hayo, kilikaa kikao cha Kamati ya Tembo na Faru mjini Dodoma ambacho kilitoa mapendekezo yake kuwa faru John anafaa kwenda Grumeti.

Miongoni mwa mambo yaliyojadiliwa ni pamoja na usalama wake, gharama kubwa za kumhamisha na suala zima la siasa kuhusu hatua hiyo.

Kwa hiyo taratibu zikaanza, ikiwamo kutafuta madaktari watakaoshiriki kumkamata, ambao miongoni mwao walikuwa kutoka Kenya.

Hatua ya kwanza ya kumhamisha kwa mujibu wa taarifa za wataalamu wa uhifadhi, ilikuwa ni kujengwa kwa banda maalumu ambalo faru John aliingizwa Novemba 7, 2015.

“Unajua kuna taratibu za kuhamisha faru, hamuwezi kumdunga sindano ya usingizi na kumbeba, unaweza kumjeruhi na hata kusababisha kifo, kwa hiyo tulimuacha azoee lile banda kwanza kwa kumuwekea miwa, wanapenda sana miwa.

“Kwa kawaida mkishabeba banda alimo na kuliingiza kwenye gari maalumu, ndipo mnamdunga sindano.

“Kwenye banda hilo alikuwa akiingia na kutoka kwa mwezi mmoja, ilipofika Desemba 8, 2015, ndipo akapelekwa eneo la Sasakwa, Grumeti,” alieleza mmoja wa wahifadhi aliyeshiriki kumhamisha faru huyo.

Mhifadhi huyo alilieleza gazeti hili kwamba kazi ya kumhamisha faru John ilifanywa na watu 56 na magari 15, na baada ya kumfikisha, timu ya madaktari ilibaki Sasakwa kwa siku saba kufuatilia maendeleo yake.

“Kule Sasakwa kwanza aliwekwa kwenye eneo dogo ili iwe rahisi kumfuatilia, lakini ilipofika Januari 8, mwaka huu, alifunguliwa na kuachwa kwenye eneo kubwa la wazi, na afya yake ilikuwa vizuri na alikuwa na mahusiano mazuri na faru jike aliyekuwa eneo hilo,” alieleza mhifadhi mwingine.

Hata hivyo, inadaiwa kuwa faru John alianza kuonekana amezubaa tofauti na uchangamfu wa awali na ilipofika Agosti 20, mwaka huu, hali yake ilibadilika na kuwa mbaya kiasi cha kusimama kwa shida, jambo linalotajwa kuwashtua hata madaktari waliokuwa wakimwangalia.

Inadaiwa alipoteza maisha usiku wa kuamkia Agosti 21.

Mhifadhi huyo alisema kuwa faru John alikufa akiwa na umri wa miaka 38, miaka mitatu zaidi ya wastani wa maisha ya faru ambao ni miaka 35.

Alisema kuwa baada ya kifo chake uchunguzi wa kitaalamu kubaini sababu za kupoteza kwake maisha ulifanyika na kuhudhuriwa na madaktari kadhaa na wanafunzi zaidi ya 50 kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA).

Miongoni wa madaktari wanaotajwa kushiriki ni Dk. Morris Kilewo (TANAPA), Dk. Ernest Mjingo (TAWIRI), Dk. Emmanuel Macha (TANAPA), Dk. Justin Samanche (TAWIRI) na Profesa Donald Mpanduji wa SUA.

Taarifa nyingine zinasema kuwa baada ya uchunguzi huo, pembe mbili za faru John zilikabidhiwa kwa Mhifadhi wa Ikorongo-Grumeti, ambaye ni mtumishi wa wizara ili kuzipeleka Dar es Salaam ambako nyara za Serikali zinahifadhiwa katika jengo la Makao Makuu ya Wizara ya Maliasili na Utalii (Mpingo House).

Pia pembe kubwa ya faru John ilikuwa imewekwa kifaa maalumu cha utambuzi (transponder), ambacho hadi sasa kipo ndani ya pembe hiyo, na kinachotakiwa ni kuweka betri na kupata taarifa kuhusu faru huyo, njia ambayo inatajwa kuwa bora kuliko vipimo vya vinasaba (DNA).

Baadhi ya wahifadhi ambao wamehojiwa na kikosi kazi maalumu kilichoundwa na Serikali kuchunguza kile kinachotajwa kuwa “utata kifo cha Faru John”, walisema suala hilo lilipaswa kufanywa na wataalamu wa wanyamapori.

“Jamani hili suala ni la kitaalamu zaidi, sasa tulitarajia iundwe timu ya wataalamu waliobobea katika masuala ya wanyamapori ifanye kazi kwanza, kisha kama kutaonekana kuna kosa la jinai, sasa kikosi kazi kingeingia kazini kuchunguza,” alisema mmoja wa wahifadhi waliohojiwa.

Desemba 6, mwaka huu akiwa ziarani mkoani Arusha, Waziri Mkuu aliuagiza uongozi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, umletee nyaraka zote zilizotumika kumhamisha faru John kutoka hifadhi hiyo ifikapo Alhamisi, Desemba 8.

Waziri Mkuu alitoa agizo hilo alipotembelea ofisi za Makao Makuu ya NCAA zilizopo wilayani Ngorongoro, mkoani Arusha na kuzungumza na watumishi wa mamlaka hayo pamoja na wajumbe wa Baraza la Wafugaji, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi mkoani humo.

Saa 7 usiku Desemba 9, Waziri Mkuu alipokea taarifa inayoelezea utaratibu uliotumika kumhamisha faru John kutoka Hifadhi ya Ngorongoro kwenda Sasakwa Black Rhino Sanctuary iliyoko katika Hifadhi ya Grumeti.

Akizungumza katika kikao kilichofanyika nyumbani kwake Oysterbay, Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Maghembe na baadhi ya watendaji wa wizara yake, Waziri Mkuu alisema taarifa hiyo itafanyiwa kazi na wataalamu wa ofisi yake.

Akisoma taarifa hiyo mbele ya Waziri Mkuu, Profesa Maghembe alisema hadi kufikia Desemba 2015 wakati faru John anahamishwa, alikuwa na watoto 26 (sawa na asilimia 70.2) ya faru wote waliokuwapo ndani ya kreta.

“Kati ya faru 37 waliokuwapo ndani ya kreta, watoto wake walikuwa 26 sawa na asilimia 70.2. Uamuzi wa kumwondoa John ulikuwa ni muhimu, ili kuwezesha kuongezeka kwa faru weusi na kupunguza tatizo la ‘inbreeding’ ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro.”

Baada ya kuhamishiwa Sasakwa, Waziri Maghembe alisema Julai 10, mwaka huu afya ya faru John ilianza kudorora na alikufa Agosti 18, mwaka huu. Taarifa hiyo iliandaliwa na Kamati ya Taifa ya Kuwalinda Tembo na Faru.

Akikabidhi pembe za faru huyo mbele ya Waziri Mkuu, Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Kitengo cha Kupambana na Ujangili wa Wanyamapori, Robert Mande, alimweleza kwamba pembe kubwa ya faru John ilikuwa na uzito wa kilo 3.6 na ndogo ilikuwa na uzito wa kilo 2.3.

Mbali ya Waziri Mkuu kupokea ripoti na pembe za faru huyo, lakini siku tatu baada ya agizo hilo, maofisa watano wa NCAA wanaotuhumiwa kushiriki kumwondoa faru John kutoka katika kreta hiyo walikamatwa kwa mahojiano, ili kujua ukweli kuhusu mazingira ya kupotea kwake.

Pia Waziri Mkuu aliituhumu menejimenti na wafanyakazi wa NCAA kuwa imejaa vitendo vya rushwa na wizi na asingeweza kuvumilia sakata la faru John, ambaye alisema kuwa aliuzwa kwa Sh milioni 200 kwenye Hoteli ya Grumeti iliyo Hifadhi ya Serengeti na kuwa walipokea fedha za awali Sh milioni 100.

Waziri Mkuu alisema anataka kumwona faru huyo, nyaraka za kumhamisha na kama amekufa basi apelekewe hata pembe ofisini kwa kuwa anajua pa kuzipeleka.

Alisisitiza kuwa ikibainika kuna ambao wamekiuka taratibu watawajibika.

Watu 6 wanaswa na silaha kwa mganga wa kienyeji Mwanza

Taarifa Ya Jeshi La Polisi Mkoa Wa Mwanza Kwa Vyombo

Kwamba Tarehe 18.10.2016 Majira Ya Saa 13:00hrs Katika Eneo La Buswelu Kata Ya Buswelu Wilaya Ya Ilemela Jiji Na Mkoa Wa Mwanza, Askari Wakiwa Katika Misako Na Doria Walifanikiwa Kuwakamata Watu Sita Wakiwa Na Silaha Mbili Zilizotengenezwa Kienyeji Pamoja Na Risasi Ishirini Na Tatu, Ambazo Walikuwa Wakizitumia Katika Matukio Ya Unyang’anyi Wa Mali Na Uporaji Hapa Jijini Mwanza Na Mikoa Mingine.

Aidha Tukio Hilo Limefanikiwa Baada Ya Kupokea Taarifa Kutoka Kwa Raia Wema Kuhusu Uwepo Wa Wahalifu Hao, Ndipo Askari Walifanikiwa Kumkamata Kwanza Jeremiah Maligia @ Mkumbo Miaka 25, Mnyiramba, Fundi Seremala Mkazi Wa Malega – Singida Ambaye Alipohojiwa Alikiri Kuhusika Na Kutaja Wenzake Waliokuwa Wakishirikiana, Na Kuwa Silaha Wamezificha Kwa Mganga Wa Kienyeji Aitwaye Leornad Litta @ Makai Anayeishi Mtaa Wa Kagida – Buswelu.

Askari Walikwenda Mahali Hapo Na Kufanikiwa Kumkamata Mganga Huyo Wa Kienyeji Bwana Leornad Litta Miaka 39, Akiwa Na  Silaha Hizo Mbili Zilizotengenezwa Kienyeji Hapo Nyumbani Kwake Na Risasi Ishirini Na Mbili Zinazotumiwa Na Bunduki Ya Aina Ya Short Gun Na Risasi Moja Ya Rifle Aina Ya Mark Iv.

Aidha Katika Kuhojiwa Zaidi  Na Askari Watuhumiwa Tajwa Hapo Juu Waliwataja Washirika Wao Wanne Ambao Walikuwa Wakishirikiana Katika Kufanya Uhalifu Ambapo Askari Walifanikiwa Kuwakamata, Ambao Ni 1. Kamgisha Jovini Kamhambwa Miaka 40, Mlinzi Na Mkazi Wa Iloganzala, 2. Juma Yusuph @ Jimi Miaka 35, Mkazi Wa Bwani Kinondoni, 3. Samweli Peter Miaka 36, Mkazi Wa Busweli Na 4. Shabani Hussein Miaka 26, Fundi Viatu Na Mkazi Wa Nyasaka Msumbiji.

Watuhumiwa Wote Walipofanyiwa Mahojiano Walikiri Kwamba Silaha Hizo Walizitumia Katika Unyang’anyi Wa Mali Na Uporaji Katika Maeneo Ya Jiji Na Mkoa Wa Mwanza, Aidha Jeshi La Polisi Kwa Sasa Linaendelea Na Uchunguzi Kuhusiana Na Tukio Hilo Na Matukio Waliyokuwa Wameyafanya, Pindi Uchunguzi Ukikamilika Watuhumiwa Wote Watafikishwa Mahakamani.

Kamanda Wa Polisi Mkoa Wa Mwanza Naibu Kamishina Wa Polisi Ahmed Msangi Anatoa Wito Kwa Wakazi Wa Jiji Na Mkoa Wa Mwanza Akiwataka Kuendelea Na Tabia Ya Kutoa Ushirikiano Kwa Jeshi Lao La Polisi, Ili Tuweze Kudhibiti Uhalifu Katika Mkoa Wetu., Lakini Pia Anatoa Angalizo Kwa Wananchi Haswa Vijana Akiwataka Kuacha

Tabia Ya Kujihusisha Na Uhalifu Bali Wajikite Katika Kufanya Shughuli Halali Za Maendeleo, Kwani Jeshi La Polisi Lipo Vizuri

Kuhakikisha Ulinzi Na Usalama Upo Kwa Raia Wote Wa Jiji Na Mkoa Wa Mwanza.

Katika Tukio La Pili

Mnamo Tarehe 18.10.2016 Majira Ya Saa 14:00hrs Mchana Katika Eneo La Ilemela Wilaya Ya Ilemela Jiji Na Mkoa Wa Mwanza, Askari Walifanikiwa Kuwakamata Watu Wawili Ambao Ni 1. Rahim Feka Miaka 28, Mkazi Wa Ilala – Dar Es Salaam, 2.  Ally Kawalale Miaka 32, Mkazi Wa Jetrumo – Arport Dar Es Salaam, Wakiwa Wanataka Kuuza Gari Lenye Namba T.778 Azv Aina Ya Toyota Land Cruiser Lililokuwa Wameliiba Huko Ilala Jijini Dar Es Salaam.

Aidha Watuhumiwa Hao Walikamatwa  Baada Ya Kupokelewa Taarifa Ya Kuibiwa Kwa Gari Hilo Huko Dar Es Salaam Na Kwamba Kuna Uwezekano Kuwepo Eneo La Kanda Ya Ziwa, Ndipo Ulifanyika Upelelzi Kuhusiana Na Taarifa Hiyo, Na Kufanikiwa Kuwakamata Watuhumiwa Tajwa Hapo Juu Wakiwa Na Gari Hilo.

Watuhumiwa Wote Wapo Chini Ya Ulinzi Wa Jeshi La Polisi Wakiendelea Na Mahojiano , Huku Taratibu Za Kuwasafirisha Kwenda Dar Es Salaam Wakiwa Chini Ya Ulinzi  Wa Askari Polisi Zikiwa Bado Zinaendelea.

Kamanda Wa Polisi Mkoa Wa Mwanza Naibu Kamishina Wa Polisi Ahmed Msangi Anatoa Rai Kwa Wakazi Wa Jiji Na Mkoa Wa Mwanza Akiwataka Kuacha Tabia Ya Kununua Vitu Vya Wizi, Bali Pindi Wanapoona Biashara Za Wizi Zinataka Kufanyika Au Zinafanyika Watoe Taarifa Polisi Ili Watuhumiwa Waweze Kukamatwa Na Kufikishwa Mahakamani.

Katika Tukio La Tatu

Kwamba Tarehe 18.10.2016 Majira Ya Saa 23:00hrs Katika Kitongoji Cha Ibungiro Kijiji Cha Sagani Kata Ya Kandawe Wilaya Ya Magu Mkoa Wa Mwanza, Mtu Mmoja Msichana Aliyejulikana Kwa Jina La Dema Charles @ Bulayi Miaka 20, Mkazi Wa Kandawe, Ameuawa Kwa Kukatwa Na Vitu Vyenye Ncha Kali Sehemu Za Kichwani Na Kiunoni

Akiwa Amelalala Na Watu Wasiojulikana, Huku Wenzake Wa Wili Wakijeruhiwa Sehemu Mbalimbali Za Miili Yao.

Majeruhi Waliojeruhiwa Katika Tukio Hilo Ni 1.mariam Lucas @ Kapele Miaka 26, Mkazi Wa  Kijiji Cha Sagani Aliyejeruhiwa  Shingoni Na Kwenye Kiganja Cha Mkono Wa Kulia, 2. Kapelele Makubi @ Salulo Miaka 90, Ambaye Ni Baba Mwenye Nyumba/ Mji, Aliyejeruhiwa Mgongoni, Kichwani Na Kiunoni.

Inadaiwa Kuwa Wauaji Hao Walifika Katika Nyumba Hiyo Majira Tajwa Hapo Juu Na Kuwakuta Wenye Mji  Wakiwa Wamelala, Ndipo Waliingia Ndani Na Kufanya Mauaji Hayo, Hadi Sasa Hakuna Mtu Yeyote Aliyekamatwa Kuhusiana Na Tukio Hilo.

Aidha Uchunguzi Wa Awali Umebainisha Kuwa Mauji Hayo Yametokana Na Kulipiza Kisasi, Jeshi La Polisi Kwa Sasa Lipo Katika Upelezi Pamoja Na Uchunguzi Kuhusiana Na Tukio Hilo, Majeruhi Wapo Katika Hospitali Ya Wilaya Ya Magu Wakiendelea Kupatiwa Matibabu Na Hali Zao Zinaendelea Vizuri.

Kamanda Wa Polisi Mkoa Wa Mwanza Naibu Kamishina Wa Polisi Ahmed Msangi Anatoa Wito Kwa Wakazi Wa Jiji Na Mkoa Wa Mwanza Akiwataka Kutoa Ushirikiano Kwa Jeshi La Polisi Ili Watuhumiwa Wa Mauaji Hayo Wawezwe Kukamatwa Na Kufikishwa Katika Vyombo Vya Sheria.

Imetolewa Na:

Dcp: Ahmed Msangi

Kamanda Wa Polisi (M) Mwanza

Majambazi Hatari Wauawa.....Bunduki 9 Zakamatwa

Jeshi la polisi limedai kwamba limeua majambazi wawili  hatari na kukamata bunduki tisa, kati ya hizo SMG saba, shotgun moja na riffle moja, risasi 473 na magazini 16 baada ya majibizano ya risasi katika misitu ya Milima ya Usambara, Kijiji cha Magamba wilayani Lushoto. 
Katika majibizano hayo, pia polisi walidai kukamata bendera zenye maandishi ya lugha ya Kiarabu, redio saba za upepo na soksi za kuficha nyuso.
 
Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Polisi, Nsato Marijani alisema jana kuwa hiyo ilikuwa operesheni ya kuwasaka majambazi waliovamia Chuo Kikuu cha Sekomu, wilayani humo hivi karibuni.
Alisema katika tukio hilo, askari wawili walijeruhiwa kwa risasi. Marijani ambaye alikuwa katika milima hiyo inayodaiwa kuwa ngome ya majambazi hao, aliwataja waliouawa kuwa ni Mudrick Abdi (24) maarufu kwa jina la Osama, mkazi wa Mbagala Majimatitu Dar es Salaam na Sultan Abdallah (24) mkazi wa Kiembesamaki, Zanzibar. 
Alisema askari waliojeruhiwa wanaendelea na matibabu na kwamba hawakupata madhara makubwa kwa kuwa walikuwa wamevaa majaketi ya kuzuia kupenya risasi .

Waziri Kairuki Afanya Ziara Dar, Kinondoni Kukagua Mradi Wa TASAF.......Asisitiza Waliotafuna Fedha Hizo Watatumbuliwa

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angella Kairuki amesema atahakikisha anawachukulia hatua watendaji wote, walioshiriki katika udanganyifu wa kuingiza kaya zisizostahili katika Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini unaosimamiwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf).

Aidha, aliiagiza Tasaf kuhakikisha inafuatilia kaya zote ambazo ziliingizwa katika mpango huo bila kuwa na sifa zinazostahili, kwa kuziorodhesha kwa majina, wanapoishi na kiasi cha fedha walichopokea ili ripoti hiyo iwasilishwe kwa Rais John Magufuli.

Kairuki aliyasema hayo jana wakati akizungumza baada ya kupokea ripoti ya utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini (Tasaf III) ya Mkoa wa Dar es Salaam, sambamba na kuzungumza na wananchi katika mitaa ya Kigogo Kati na Mikoroshoni, Manispaa ya Kinondoni.

“Kaya ambazo hazistahili hawafanyi peke yao wanashirikiana na watu, kama ni viongozi katika ngazi za mitaa na kata mitaa tunataka majina, na katika kila jina tujue nani alishiriki kumuingiza nani alikuwa akimchukulia na kama yupo mtumishi wetu wa umma tujue ni nani na hatua gani za kinidhamu zimechukuliwa.”
 “...Msije mkashangaa nikaja kuelekeza polisi kukamata hawa na hawa kwa sababu hizi hela ni lazima zirudi,” alisema Kairuki.

Alisema ameshapokea taarifa za mikoa mbalimbali, lakini Dar es Salaam na wilaya zake bado na mwisho ilikuwa ni Oktoba 6, mwaka huu, lakini aliwaongeza wiki moja ambayo tayari imeisha na orodha hiyo inatakiwa ipelekwe kwa Rais Magufuli.

Kairuki aliongeza kuwa pamoja na mkoa kusema umeondoa kaya 789 ambazo hazina sifa, lakini kuna kaya 5,457 ambazo zinapaswa kuondolewa katika mpango huo kwa kuwa hazina sifa za kupokea ruzuku hiyo. 
“...baada ya kuelekeza uhakiki wa nyumba kwa nyumba, sisi kwa taarifa tulizonazo tutaondoa kaya 5,457. Sasa ujiulize nyinyi ndio mlikuwa katika zoezi na mkapata idadi hiyo, hapa inaonesha kuna kitu hakipo sawa,” alisema.

Alisema katika kaya hizo zitakazoondolewa, 1,867 hazina vigezo vya umasikini, 563 zipo kwenye orodha lakini zilikuwa hazijitokezi kuchukua ruzuku na hazijulikani zilipo na kaya nyingine 2,114 hazikupatikana wala kujulikana zilipo wakati wa ukaguzi.

Alisema kaya hizi ni nyingi na hasa ikizingatiwa asilimia 76 hazijaingizwa katika mpango huo, hivyo kaya hizo ambazo ziliandikishwa zinapaswa kwenda kukaguliwa ili ziweze kuingizwa katika mpango huo ili katika awamu ya nane ya uhawilishaji fedha waweze kupata.

Kairuki alisema kiasi kikubwa cha fedha kimepotea, ambacho kingeweza kuwasaidia watu wanaostahili kuwa katika mpango huo. 
Alisema wilaya za Kinondoni na Temeke zimeshapokea malipo ya awamu saba ambayo ni Sh bilioni 6.7. Alisema hadi sasa kuna kaya 32,456 zilizoondolewa kwenye mpango huo.

Kwa wastani kaya moja hulipwa kati ya Sh 20,000 hadi 60,000 kwa kutegemea idadi ya watu katika kaya.

Akizungumza katika mkutano huo, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ali Hapi ambaye pia ni Kaimu Mkuu wa Mkoa alisema mpango huo ni muhimu kwa maendeleo ya taifa, lakini kuna watu wanaoharibu taswira ya Tasaf.

Alisema kuna fedha nyingi ambazo zinaishia kwenye mikono ya wajanja na haziwafikii walengwa wa mpango huo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Tasaf, Ladislaus Mwamanga alisema mpango huo umeandaliwa kitaalamu na utaendelea kuwa endelevu na kwamba mradi huo unategemea zaidi serikali na wafadhili, lakini hadi sasa kiasi kikubwa kimekuwa kikitoka kwa wafadhili.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa umma na Utawala bora Mh. Angela Kairukia akiwa sambamba na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,akiendelea na ziara katika Mkoa wa Dar es salaam kukagua maendeleo ya mradi wa kusaidia kaya masikini TASAF

Nyota ya Godbless Lema Inavyomng'arisha RC Gambo Mbele ya Rais Magufuli

Kama mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema anapambana na Mrisho Gambo ili kujijenga kwa wananchi wake, basi mkuu huyo wa mkoa ananufaika na vita hiyo na anatarajia makubwa zaidi baada ya mzozo wa mwanzoni mwa wiki.

Wakati Gambo akitarajia kupandishwa cheo na Rais John Magufuli, madiwani wa jiji hilo wametangaza kususia vikao vyote hadi viongozi wa juu wa Serikali watakapoingilia kati mgogoro uliopo.

Wawili hao waliingia kwenye mzozo mwingine mapema wiki hii wakati Gambo alipoalikwa kuzindua ujenzi wa hospitali ya mama na mtoto, itakayojengwa kwa ufad kwa ufadhili wa taasisi ya Martenity Africa alipojaribu kueleza historia ya kiwanja cha jengo hilo, maelezo ambayo Lema aliyapinga kwa sauti kubwa na kusababisha shughuli hiyo kuvurugika.

Baada ya mzozo huo, Gambo amedokeza kuwa kuna makubwa yanafuata.

“Baada ya hilo, simu zilikuja kibao, lakini bahati nzuri kabla sijauliza kokote, na Mheshimiwa Rais ndio akawa ananipigia akaniambia nina full confidence (nina imani) na wewe. Labda wafikirie promotion (kupandisha cheo), lakini hayo mengine hayapo,” alisema Gambo akiwaeleza wafanyabiashara wa mjini hapa kuhusu barua iliyosambaa juzi kwenye mitandao ya kijamii kuwa Rais ametengua uteuzi wake.

“Baadaye (Rais) akaniambia kwamba sasa ili (wafanyabiashara) wajue kwamba kweli nimekupigia simu, niitie mmoja uliye naye karibu ili niongee naye. Ndio (mwenyekiti wa wafanyabiashara wa Arusha) akapata previledge (bahati) naye ya kuongea na Mheshimiwa Rais.”

Iwapo Gambo atapandishwa cheo, ambacho kwa mukhtadha wa utumishi wa umma chaweza kuwa ni kuteuliwa kuwa mbunge na baadaye waziri, itakuwa ni mara ya pili kupanda cheo siku chache baada ya kuzozana na Lema.

Gambo, ambaye aliteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha Juni 26, alilumbana na Lema Agosti Mosi mbele na Naibu Waziri wa Tamisemi, Suleiman Jafo.

Katika tukio hilo, Lema alisema Gambo haheshimu mipaka ya kazi zake, akimtuhumu kuingilia maamuzi ambayo tayari yameshajadiliwa kwenye vikao halali vya halmashauri na kupitishwa na ofisi ya mkuu wa mkoa katika kikao cha wakuu wa idara, maofisa tarafa, waratibu wa elimu kata watumishi wa Mamlaka ya Maji Safi na Mazingira (Auwsa) jijini hapa.

“Nimeona nizungumze hapahapa ili naibu waziri ufahamu hali ilivyo hapa. Kwa mfano Baraza la Madiwani la mwaka 2008, ndilo lililopitisha kiwango cha posho kwa madiwani kutoka Sh100,000 hadi 120,000. Jambo la kushangaza DC ameandika barua Tamisemi na nakala kwa Takukuru ili wachunguze jambo ambalo limeshapata baraka za Tamisemi,” alisema Lema.

Hali hiyo ilimfanya naibu waziri kuingilia kati na kuahidi kuzishughulikia changamoto hizo na kumpa nafasi Gambo, ambaye wakati huo alikuwa mkuu wa wilaya, kujibu hoja hizo. 
“Mheshimiwa mbunge nataka ujue mimi ndiyo mkuu wa shughuli za Serikali hapa wilayani. Muda wowote nina uwezo wa kuingilia kati mambo ambayo naona hayaendi sawa, hata kama yupo katibu tawala na viongozi wengine,” alisema Gambo.

“Rais aliona ninafaa ndiyo maana akaniteua na sihitaji kujifunza namna ya kuwa mkuu wa wilaya  kwa kuwa huu ni mwaka tano.”

Malumbano hayo yaliendelea na kumuhusisha pia Meya wa Jiji la Arusha, Calist Lazaro ambaye aliungana na Lema na madiwani wengine kupinga jambo hilo.

Baada ya vuta nikuvute hiyo mbele ya waziri, Agosti 18 Gambo aliteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha kuchukua nafasi ya Felix Ntibenda.

Siku chache baada ya uteuzi huo, Gambo aliagiza halmashauri ya jiji kutafuta fedha za kupunguza deni la walimu ambalo ni Sh154 milioni. 
Mkurugenzi wa jiji hilo, Athuman Kilamia alitangaza posho za madiwani ambazo zilikuwa zinalipwa kinyume cha taratibu, zitumike kupunguza deni la walimu na zikatolewa.

Mgogoro ukaibuka kati ya madiwani wa jiji hilo ambao wengi ni kutoka Chadema.

Sakata la Jumanne wiki hii linaweza kumpa cheo kikubwa zaidi kutokana na Rais Magufuli kumpigia simu kwa lengo la kumthibitishia kuwa yuko pamoja naye siku ambayo barua ya kughushi ilisambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa mkuu huyo wa nchi ametengua uteuzi wa Gambo.

Sakata hilo lilitokea katika uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa hospitali ya mama na mtoto jijini Arusha ambao utagharimu Sh9 bilioni, sehemu kubwa ya fedha hizo zikitoka taasisi ya Martenity Africa.

Mvutano huo ulianza baada ya Gambo kusema kuwa ardhi kwa ajili ya ujenzi wa hospitali imetolewa na Taasisi ya Mawalla Fund kwa kuwa muasisi wake, Nyaga Mawalla alikuwa na maono ya kusaidia afya ya mama na mtoto.

Kauli yake ilikuwa ikimaanisha kuwa Mfuko wa Maendeleo wa Arusha (ArDF) haikutoa kiwanja hicho kwa Martenity Africa wala kutafuta mfadhili.

Jambo hilo liliwakera viongozi wa ArDF, ambayo imeanzishwa na Lema na Elifuraha Mlowe, ambaye ni mwenyekiti. 
Lema alimtaka ndugu wa wakili huyo amsahihishe Gambo, lakini hakuna kilichofanyika, ndipo aliposimama na kuanza kupinga kwa sauti maelezo ya Gambo.

Lema alikuwa akisema mkuu huyo wa mkoa anapotosha ukweli kwa misingi ya kisiasa, kwa kuwa Mawalla Fund ilitoa kiwanja hicho kwa ArDF, ambayo ilitafuta wafadhili na kusaini nao mkataba wa ujenzi wa hospitali.

Wageni kwenye hafla hiyo iliyofanyika Bulka walijaribu kuwatuliza wawili hao, hawakufanikiwa kutokana na Lema kuendelea kueleza kwa sauti kuwa Gambo anapotosha, huku mkuu huyo wa mkoa akizungumza kwenye kipaza sauti kumtaka mbunge huyo atulie.

Shughuli hiyo ilimalizika kiutata na hivyo waandaaji wakashindwa kuendesha harambee iliyopangwa kufanyika baada ya uzinduzi.

Serikali Yakubali Kurejesha Posho ya Sh. 8500 kwa Siku kwa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Nchini

Bodi ya Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetuliza hasira za wanafunzi wa vyuo vikuu kwa kurejesha posho ya chakula na malazi ya Sh8,500 kwa kila mmoja na kwamba tofauti baina yao itakuwa viwango vya ada.

Ufafanuzi huu uliotolewa jana usiku na Waziri wa Elimu, Sayansi , Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Profesa Joyce Ndalichako wakati akizungumza katika mahojiano maalimu na kituo cha runinga cha Taifa -TBC utakuwa faraja kwa wanafunzi ambao chini ya Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Daruso) walipanga kushinikiza walipwe posho ya Sh8,500 kwa siku kama ilivyokuwa awali. 
 
Hatua ya wanafunzi kujenga umoja ili kushinikiza haki katika posho ilitokana na baadhi yao kuingiziwa kati ya Sh40,000 na 70,000 badala ya Sh 510,000, hali ambayo ilizua sintofahamu. 
Ndalichako alisema tofauti ya malipo itakuwa katika ada na siyo posho, “Vigezo vya mikopo vimebadilika, kila mwanafunzi atapata fedha tofauti lakini tumefanya marekebisho kwenye posho ya chakula ambayo kila mwanafunzi atalipwa Sh8,500 kama awali.” 
Kwa mujibu wa utaratibu wa Bodi hiyo, malipo hayo ya chakula na malazi hutolewa kila baada ya miezi miwili. 

Mapema jana, Daruso iliwataka wanafunzi wa chuo hicho kutotia saini fomu za fedha za mikopo yao mpaka itakapowapa ruhusa ya kufanya hivyo. 
Rais wa Daruso, Erasmi Leon alisema hayo jana wakati akizungumza na wanafunzi wenzake kuhusu kusudio la kwenda HESLB kwa ajili ya kutafuta haki yao ya msingi. 
“Ninachowasihi tuwe pamoja. Tuwe wamoja na twende pamoja. Tutakwenda wawakilishi kutafuta nafasi kwa amani waweze kusikia tuna hoja gani lakini tukinyimwa hii nafasi tutaenda kuitafuta tukiwa wengi,” alisema na kuongeza:
 “Tuwe watulivu kwa sasa tutakapowahitaji muda na wakati wowote kwa lolote tushirikiane ili twende pamoja tumalize pamoja tuhakikishe tunapata Sh8,500 kwa kila mwanafunzi kwa chakula na malazi,” alisema. 
Kuhusu suala hilo, uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ulisema wajibu wake ni kupokea na kusambaza majina na taarifa kutoka Bodi kwa wanafunzi. 
Akitoa ufafanuzi kwa wanafunzi waliofika ofisini kwake kujua hatima yao na waliopata mikopo kuchukua fomu za kutia saini, Ofisa Mikopo wa UDSM, Lugano Mwakyusa alisema wenye jukumu la kujua walio na sifa ya kupata mikopo ni Bodi ya Mikopo. 
“Tunaendelea kupokea majina kutoka bodi. Tayari hapa kuna majina 949 yameshatoka, wengine tuzidi kusubiri na wale mwaka wa pili na tatu ambao walikuwa na mitihani ya marudio taarifa zao zitapelekwa bodi,” Mwakyusa aliwaambia wanafunzi waliokuwa wamejaa ofisini kwake.
 Kulikuwa na hali ya sintofahamu chuoni hapo jana baada ya wanafunzi wengi wa mwaka wa kwanza kuonekana wakiwa wameshika bahasha za kaki zilizokuwa na fomu za usajili wanazotakiwa kujaza huku wakihangaika kutokana na kutojua kiasi cha mkopo. 
Juzi, Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, AbdulRazaq Badru alieleza kwamba ingawa wanafunzi 88,000 waliomba mikopo kutoka HESLB, uwezo wa bodi hiyo ni kutoa kwa wanafunzi 21,500 pekee sawa na asilimia 24 na waliokuwa wameshapatiwa walikuwa 11,000 sawa na asilimia 12. 
Takwimu hizi zinaonyesha zaidi ya robo tatu ya wanafunzi wanaohitaji mikopo watakosa kutokana na uwezo mdogo wa kifedha.

Kikosi Kazi Cha Jeshi La Wananchi (JWTZ) Cha Wasili Kagera Kwa Ajili Ya Kujenga Miundombinu Iliyoathiriwa Na Tetemeko La Ardhi

Kikosi kazi cha jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ)kutoka makao makuu ya Jeshi kimewasili Mkoani Kagera kwaajili ya ujenzi wa miundombinu ya serekali iliyoathiriwa vibaya na tetemeko la ardhi lililotokea Mkoana Kagera septemba 10 mwaka huu.

Akiongea wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa kituo cha afya katika kijiji cha Kabambyaile Kata ya Ishozi Wilaya ya Missenyi, Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali mstaafu Salum Kijuu alisema kuwa kikosi hicho kinawataalamu wa fani zote za ujenzi na wamekuja na vifaa vyote vya ujenzi.

"Hiki kikosi kitafanya kazi kwa masaa 24 yaani watajenga usiku na mchana taasisi zote za umma zilizoathiriwa na tetemeko ikiwa ni pamoja na mashule na zahanati ili watoto waende shule na wagonjwa waendelee kupata matibabu"alisema.
Alisema mpaka kufikia july mwakani ujenzi wa miundombinu utakuwa umekamilika kwa robo tatu na aliwataka wananchi wawape ushirikiano maeneo yote watakayopita kujenga miundombinu ya umma.

Kiongozi wa kikosi hicho Meja Buchadi Kakura alisema kuwa kikosi hicho kimekuja Kagera kusaidia serekali ya Mkoa kurudisha miundombinu yote ya umma iliyoathiriwa na tetemeko la ardhi katika hali yake ya kawaida.

"Ni vigumu kusema lini tutakamilisha ujenzi ila sisi tutafanya kazi usiku na mchana ili ujenzi huu ukamilike ndani ya muda mfupi"Alisema Meja Kakura.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali mstaafu Salimu Kijuu(mwenye Suti)akisikiliza maelezo juu ya kikosi kazi cha askari waliokuja kujenga miundo mbinu ya umma iliyoathiriwa na tetemeko la ardhi

Mwamuzi Aliyepigwa Tanga Atoka Hospitali

fujo-1 
YULE mwamuzi aliyechezea kichapo kutoka kwa mashabiki wa Coastal Union, Jumapili iliyopita, Thomas Mkombozi ameripotiwa kuendelea vizuri kiafya baada ya kupatiwa matibabu hospitali na amesharuhusiwa kutoka.
Mkombozi alipata mkong’oto huo kwa kupigwa na magongo na makonde kutoka kwa mashabiki hao mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza baina ya Coastal ya Tanga dhidi ya KMC ya Dar es Salaam, uliopigwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga. Coastal ilifungwa mabao 3-2.
Msimamizi wa Kituo cha Tanga, Khalid Abdallah ameliambia Championi Jumatano kuwa tetesi zinazosambaa kuwa mwamuzi huyo alipoteza fahamu na hakujitambua mpaka alipofika hospitali si za kweli na kwamba alifanyiwa matibabu siku hiyohiyo kwa kushonwa jeraha lake la kichwani na kuruhusiwa.
“Mimi nilikuwa naye (Mkombozi) tangu tunampelekea hospitali, mpaka anatibiwa na kushonwa kichwani kutokana na jeraha alilopasuka kichwani, akaruhusiwa kwa maana hakukuwa na haja ya kulazwa kutokana na hali yake, baada ya hapo tukaenda polisi na kisha hotelini kwake.
“Si kweli kwamba alizimia, alikuwa anaelewa kila kitu kinachoendelea, kwa sababu tulikuwa na waamuzi wengine na tulikuwa tunaongea naye kama kawaida, isipokuwa tunaweza kusema anaumwa kutokana na majeraha lakini kwa kifupi yupo vizuri na anaendelea vizuri kwa sasa,” alisema Khalid.
Kutokana na tukio hilo, tayari Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kupitia kwa Ofisa Habari, Alfred Lucas, limeweka wazi kuchukuliwa hatua na kutolewa maamuzi na Kamati ya Saa 72.
Na Hans Mloli, Dar es Salaam

Watumia Jina la Tibaijuka Kutapeli

MBUNGE wa Muleba Kusini, Profesa Anna Tibaijuka amehadharisha umma dhidi ya ukurasa uliotengenezwa katika mtandao wa kijamii wa Facebook ukitumia jina lake, kuwa anakaribisha maombi ya watu wa kuajiriwa kwenye shirika linalosaidia watu kuondokana na umasikini.

Profesa Tibaijuka ambaye amesisitiza kuwa ukurasa huo si wake, ametaka taarifa zilizomo zipuuzwe akisema umetengenezwa na matapeli wanaochafua jina lake ambao wanadai watu watakaopitishwa, watapata fursa ya kufanya kazi katika nchi mbalimbali Afrika.

“Ukurasa huu sio wa kwangu wala siufahamu. Hivyo basi na taarifa zote zilizoandikwa kwenye ukurasa huu ni uongo na hazitoki kwangu…nawaomba mpuuze taarifa hizi na wala msitume taarifa zenu kupitia parua pepe kama inavyoelekeza,” Profesa Tibaijuka aliliambia gazeti hili jana.

Taarifa zilizopo kwenye ukurasa huo, zinakaribisha watu kutuma maombi ya kufanya kazi na shirika lisilo la kiserikali (NGO) linaloshughulika na kupunguza umasikini uliokithiri katika Afrika.

Wenye uhitaji wanatakiwa kutuma taarifa kwenye barua pepe iliyoonesha jina la Profesa Tibaijuka huku ikielezwa kuwa sifa zinazotakiwa ni kuanzia elimu ya sekondari na kwamba wanaohitaji wawe tayari kufanya kazi katika nchi nyingine za Afrika.

Aidha, taarifa hizo zinasisitiza kuwa wanachama wa skauti na klabu ya Lions watapewa kipaumbele. Mbunge huyu aliyewahi kuwa Mkurugenzi wa Shirika la Makazi Duniani (UN-Habitat), alisema taarifa juu ya utapeli huo zimekwishavifikia vyombo vya usalama na wanaendelea na uchunguzi kubaini na kuwakamata mara moja wahusika.

Jeshi la Polisi Dar Laua Majambazi Hatari 6

Watu sita wanaotuhumiwa kuwa majambazi hatari, wameuawa katika majibizano ya risasi na Polisi katika eneo la Mbezi kwa Yusuf Makondeni katika Manispaa ya Kinondoni, Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa Kanda Maalumu, Naibu Kamishna wa Polisi, Lucas Mkondya, watuhumiwa hao waliuawa katika majibizano ya risasi na Kikosi Maalumu cha Kupambana na Ujambazi wa Kutumia Silaha.

Mkondya alisema wamepata taarifa kutoka kwa raia mwema kuwa kuna kikundi cha watu wenye silaha, wamejipanga kufanya tukio la ujambazi kwa kutumia silaha kwa mfanyabiashara aliyekuwa akitoka Benki ya Diamond Trust Bank (DTB), tawi la Barabara ya Nyerere, ambaye angepita katika barabara hiyo kwenda mkoani Morogoro.

Alisema baada ya kupata taarifa hizo, polisi waliweka mtego na majambazi hao wakitumia gari aina ya Toyota Carina lenye namba za usajili T970 DGZ rangi ya fedha, walionekana wakilifukuza gari la mfanyabiashara huyo, kisha kulipita na kumsimamisha kwa nguvu.

“Majambazi wawili wakiwa na bastola walishuka katika gari hilo. Baada ya kugundua kuwa wameingia kwenye mtego wa polisi, walianza kufyatua risasi kwa askari wakitumia bastola na wenzao waliokuwa wamejaa kwenye gari yao walianza kushuka huku wakifyatua risasi kuelekea kwa askari,” alisema Kaimu Kamanda Mkondya.

Alisema kutokana na hali hiyo, askari walianza kujibu mashambulizi na kuwaua majambazi hao na baada ya upekuzi, zilipatikana bastola mbili, moja ya kijeshi aina ya Chinese ikiwa na risasi moja ndani ya kasha la risasi; na nyingine aina ya Browning ikiwa imefutwa namba zake na maganda sita ya risasi yaliyookotwa katika eneo la tukio.

Miili ya watuhumiwa hao imehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na upelelezi unaendelea ili kubaini mtandao mzima wa ujambazi.

Katika tukio lingine la Oktoba 17, mwaka huu saa 2:00 usiku katika maeneo ya Tegeta Masaiti, watuhumiwa watatu wa ujambazi wakiwa wamepakizana kwenye pikipiki aina ya Fekon yenye namba MC370 BEY, wakiwa na bunduki aina ya shotgun iliyokatwa mtutu na kitako, walivamia duka la Abdallah Juma (46), mkazi wa Tegeta na kupora fedha za mauzo na kuiba vocha za mitandao mbalimbali, ambazo thamani yake haijafahamika.

“Polisi baada ya kupata taarifa waliwafukuza majambazi hao, walipoona wanakaribiwa na askari, walitupa chini begi walilokuwa nalo na kutelekeza pikipiki yao kisha kukimbia, begi lilipopekuliwa lilipatikana na silaha hiyo,” alisema.

Aidha, wananchi wenye hasira waliendelea kuwakimbiza majambazi hao na kumuua mmoja huku wengine wakikimbilia kusikojulikana.

Katika hatua nyingine, Mkondya alisema wamekamata watuhumiwa wawili wa unyang’anyi kwa kutumia nguvu wakiwa na pikipiki moja na funguo bandia 75.

Alisema watuhumiwa hao, Ally Makwega (53) mkazi wa Tandika na Fabian Greyson (39) mkazi wa Yombo walikamatwa Oktoba 4, mwaka huu saa 6:00 usiku.

Watuhumiwa hao walikamatwa wakiwa na pikipiki yenye namba MC292 AMD aina ya Boxer rangi nyekundu, wanayoitumia kufanya uhalifu, wakiwa na funguo bandia 75 ambazo huzitumia katika kuvunja nyumba mbalimbali ya biashara za kulala wageni, maghala ya kuhifadhia bidhaa na maduka.

Baada ya watuhumiwa hao kuhojiwa, walikiri kuhusika na matukio mbalimbali ya uvunjaji wa maghala na kuiba katika mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro na Dodoma.

Watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.

VIDEO: Ufafanuzi alioutoa mbunge aliyedaiwa kupokea mishahara hewa ya miezi mitano


Gazeti moja la kila siku, jana liripoti likidai kuwa Mbunge wa Makete ‘CCM’, Prof. Norman Sigalla ambaye alikuwa mkuu wa wilaya ya Songea mkoani Ruvuma amekuwa akipokea mshahara wa ukuu wa wilaya kwa miezi mitano wakati alikwisha acha kazi hiyo alipoteuliwa kugombea ubunge wa Makete na kushinda.

Ilidaiwa kuwa hata baada ya kuacha kazi hiyo ya ukuu wa wilaya aliendelea kupokea mshahara wake wa ukuu wa wilaya wa milioni 4.6 kutokana na ofisa utumishi wa ofisi ya katibu tawala mkoa wa Ruvuma kumrudisha kwenye orodha ya malipo ya mshahara.

Leo kupitia kipindi cha clouds 360 cha Clouds TV, Prof Sigalla ametoa ufafanuzi wa tuhuma hizo ambapo amekanusha na kusema kiasi cha fedha kilichoingia kwenye akaunti yake kwamba si sh milionI 23 bali ni sh milioni 5 ambazo zilikuwa hazieleweki.

Hata hivyo amesisitiza kuwa baada ya kugundua kuwa pesa imeingizwa kwenye akaunti yake kabla hata ya gazeti kuripoti alimwandikia katibu wa bunge kumtaka kuanzia August akate fedha hizo kwenye mshahara wake, kuzirudisha hazina kuu na RAS achukuliwe hatua kwa kuingiza fedha kwenye akaunti isiyotumika.

VIDEO: JK Comedian alivyomchekesha mtoto wa Julius Nyerere (Makongoro Nyerere)

Msanii JK Comedian amezidi kuonyesha ubora wake katika kuziigiza sauti za watu mashuhuri kwa style ya kuchekesha, JK Comedian amekuwa akialikwa sehemu mbalimbali kuburudisha watu kwa kuiga sauti za viongozi hususani Rais mstaafu Jakaya Kikwete, hii hapa alipomuiga Rais Julius Kambarage Nyerere, Dkt John Pombe Magufuli na Jakaya Mrisho Kikwete.

Mwanafunzi Apigwa Dar, ‘Afa, Afufuka’ Mochwari

Mwanafunzi wa shule ya Sekondari Lumo wilayani Temeke, Isack Ernest alionja mauti baada ya kupigwa na wananchi kiasi cha kufikiriwa kwamba amekufa, akapelekwa chumba cha maiti ambako alizinduka.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Gilles Muroto alisema jana kwamba kijana huyo alipigwa hadi kupoteza fahamu na alipofikishwa katika Hospitali ya Rufaa ya Temeke aliwekwa kwenye chumba cha maiti pamoja na kijana mwingine aliyeuawa katika tukio hilo.

“Mwanafunzi huyo hali akiwa amelazwa pamoja na maiti nyingine zinazosubiri kuwekwa katika majokofu, alitikisika kutokana na baridi ya chumba cha maiti, wahudumu wakamwona na kumtoa, wakamvalisha nguo za maiti nyingine, akarudishwa hospitalini kwa ajili ya huduma,” alifafanua Kamanda Muroto.

Taarifa Muhimu: Serikali Yatangaza UHAKIKI wa Wanafunzi Wote Walioko Vyuo Vikuu Ambao Wanasoma Shahada

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inawatangazia Viongozi wa vyuo vyote vinavyotoa shahada nchini vya umma na vya binafsi kuwa kutakuwa na uhakiki wa ubora wa vyuo hivyo.

Uhakiki huo utaanza siku ya Jumatano Oktoba 19, 2016, hivyo, vyuo vyote vinatakiwa kutoa ushirikiano kwa timu za wataalamu zitakazofika kwa ajili ya kufanya uhakiki huo.

Aidha, katika ukaguzi wa sifa za wanafunzi wanaoendelea na masomo vyuo vyote, Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU), itatoa majina ya wanafunzi wanaotambuliwa na kwamba walidahiliwa kupitia TCU katika Programu zao za Shahada katika vyuo mbalimbali vinavyotoa shahada nchini siku ya Jumanne Oktoba 18, 2016.

Hivyo, wanafunzi wote wanatakiwa kuangalia majina yao katika Tovuti ya TCU na kwa yeyote ambaye hataona jina lake awasiliane na Uongozi wa TCU haraka iwezekanavyo ili kupata maelezo Zaidi. Mwanafunzi ambaye hatazingatia haya ndani ya wiki mbili atapoteza sifa za kuendelea na masomo.

Imetolewa na:
Katibu Mkuu
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

Mbunge Afafanua Sakata la Mishahara Mitano Hewa

Mbunge wa Makete (CCM), Profesa Norman Sigalla ambaye alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma, amekanusha kiasi cha fedha kilichoingia kwenye akaunti yake kwamba si Sh23 milioni bali ni Sh5,091,734.96 ambazo zilikuwa hazieleweki.

Profesa Sigalla alitoa maelezo hayo jana alipofika ofisi za gazeti hili, baada ya kudaiwa kupokea mshahara wa ukuu wa wilaya kwa miezi mitano wakati alikwisha acha kazi hiyo alipoteuliwa kugombea ubunge wa Makete na kushinda.

Hali hiyo, iliyoelezwa kuisababishia Serikali hasara ya Sh23 milioni, ilitokana na madai kwamba hata baada ya kuacha kazi aliendelea kupokea mshahara wake wa ukuu wa wilaya wa Sh4.6 milioni kutokana na ofisa utumishi wa ofisi ya katibu tawala wa Mkoa wa Ruvuma kumrudisha kwenye orodha ya malipo ya mshahara.

Wizara ya Mambo ya Nje yakanusha Tanzania kujitoa katika matumizi ya Viza ya Pamoja ya Utalii katika Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.


Mchakato wa kuanzisha Viza ya Pamoja ya Utalii katika Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Ndugu wanahabari:
Wiki iliyopita baadhi ya vyombo vya habari na mitandao ya jamii ya hapa nchini na nje ya nchi iliandika taarifa kuhusu Tanzania kujitoa au kugomea utaratibu wa visa ya pamoja ya utalii (Single Tourist Visa) wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Kufuatia taarifa hiyo, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imekuwa ikipokea simu nyingi kutoka kwa watu mbalimbali wakiwemo waandishi wa habari kutaka kufahamu ukweli wa jambo hilo. 


Hivyo, Wizara imeona itoe taarifa rasmi kufafanua namna ya mchakato wa uanzishwaji wa viza ya pamoja ya utalii ndani ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki unavyoendelea.

Suala la Uanzishwaji wa Viza ya Pamoja ya Utalii kwa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki bado liko katika majadiliano ya Nchi Wanachama kupitia Vikao vya Sekta ya Utalii na Wanyamapori. 
Katika kufanikisha azma hii,  Baraza la Kisekta la Mawaziri wa  Maliasili na Usimamizi wa Wanyamapori uliofanyika  tarehe 1 Novemba 2008 liliunda Kikosi Kazi kwa ajili ya kufanya  utafiti kwa lengo la kubainisha mahitaji na utayari wa Nchi wanachama juu ya kuanzisha  Viza ya Pamoja ya Utalii.  Utafiti uliofanyika mwaka 2010, ulibainisha masuala muhimu yafuatayo ya kuzingatiwa kabla ya kuanzishwa kwa Viza ya Pamoja ya Utalii:

a)Kurazinisha  (harmonization) sheria za Viza za Nchi Wanachama;
b)Idara ya Uhamiaji  kuanzisha Mfumo  wa  kudhibiti Usalama;
c)Utoaji wa Viza kuwa wa kielektroniki;
d)Kuwepo kwa mfumo wa ukusanyaji na ugawanyaji wa mapato pamoja na namna ya kulipa;
e)Kuwepo kwa maafisa uhamiaji katika kila ofisi za ubalozi;
f)Kujenga uwezo wa watumishi kwenye suala la  mfumo wa kieletroniki  wa utoaji wa viza ya pamoja ya Utalii.

Kufuatia matokeo ya utafiti huo, Mkutano wa 5 wa Baraza  la Kisekta la Mawaziri wa Utalii na Usimamizi wa Wanyamapori  uliofanyika  mwezi Julai 2013  jijini Bujumbura, Burundi pamoja na mambo mengine uliagiza kuundwa kwa kikosi kazi ambacho kitajumuisha wataalamu kutoka Taasisi za Uhamiaji, Utalii, Fedha, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Tehama, Usalama, na Sheria katika nchi wanachama ili  kuandaa mpango kazi  na  kushughulikia masuala yote ambayo  yatajitokeza kuhusiana  na uanzishwaji wa  Viza ya Pamoja ya Utalii. Hata hivyo, kabla ya utekelezaji wa maagizo hayo, Nchi za Uganda, Kenya na Rwanda zilianzisha  Viza ya Pamoja ya Utalii baina yao nje ya vikao vya Jumuiya.

Ni vema ikaeleweka kwa umma wa Watanzania na Afrika Mashariki kwa Ujumla kuwa kwa kuzingatia Mfumo wa Maamuzi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, ambao ni wa kukubaliana kwa pamoja (consensus) hakuna Mfumo wowote wa uanzishwaji wa Visa ya Pamoja ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ulioanzishwa.
 
Hii inamaanisha kuwa hakuna Visa ya Pamoja ya Utalii katika Jumuiya ya Afrika Mashariki iliyokubalika. Kwa mantiki hiyo, taarifa zilizotolewa na vyombo vya habari hazina ukweli wowote na zilikuwa na lengo la kuichafua Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inawawahakikishia umma wa Tanzania kuwa itaendelea kuheshimu maamuzi ya vikao halali vya Jumuiya na kushiriki katika majadiliano ya kuanzisha visa ya pamoja ya utalii ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Dar es Salaam, 18 Oktoba  2016.

Wateule wa Magufuli Jifunzeni Kwake Katika Kuheshimu Michango ya Watu

Nampongeza Sana Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa uwezo wake mkubwa wa Kuheshimu Michango ya watu katika jambo fulani la kimaendeleo au tu la kijamii, nitatoa Mifano michache.

1. Wakati akiwa Waziri wa ujenzi Kule Hai eneo la Kwa Sadara palikuwa na Uzinduzi wa Barabara. Mgeni Rasmi katika shughuli ile alikuwa ni Rais wa Kipindi hicho Jakaya Mrisho Kikwete.

Wakati Magufuli anatoa neno la shukrani kama Waziri Muhusika, aliona Faida ya kumpa nafasi Mbunge wa Jimbo hilo Freeman Mbowe. Nina hakika waandaaji wa hafla Ile hawakumweka Mbowe kwenye ratiba lakini Magufuli aliheshimu uwepo wake na kuuthamini na kumkaribisha aseme kidogo.

2. Mwezi April mwaka huu 2016, tayari Akiwa Rais wa Nchi. Wakati wa Uzinduzi wa Daraja la Kigamboni, Rais alikuwa mtu wa mwisho kuzungumza, aliwasikiliza wote waliozungumza kabla yake, lakini hakuna hata mmoja aliyejaribu hata kutaja Jina la Mkurugenzi aliyestaafu wa NSSF Dkt. Ramadhani Kitwana Dau. Japokuwa ni Wakati wa Uongozi wa Dau ndio shirika hilo lilifanikiwa kugharamia sehemu kubwa ya ujenzi wa Daraja hilo.

Kabla hajazungumza. Rais alimuinua Dau, akamsifia na Kuheshimu mchango wake na Taasisi aliyoiongoza. Hakuna aliyeamini macho yake pale, kila mtu aliamini kuwa Rais akikutengua katika wadhifa na kukupangia wadhifa mwengine basi wewe ni mbadhilifu au Jipu, Dau akaogopwa, hakuwekwa kwenye Ratiba akihisiwa kuwa ni Jipu, Rais akauthibitishia Umma kuwa Dau hawezi kutenganishwa na ufanikishwaji wa Daraja lile.

3. Siku ya Uzinduzi wa Mradi mpya wa kupokea simu wa Jeshi la Polisi.
Rais aliwasikiliza wazungumzaji, wote walisahau kuwa Tukio lile lilifanyikia Kinondoni na Halimashauri ya Kinondoni ipo chini ya Upinzani ikiongozwa na meya Boniface Jacob.
Rais alimuita Meya aje kusalimia, Japo meya hakuwepo lakini aliheshimiwa.

4. Jana kwenye Kuaga Mwili wa Marehemu Masaburi, Rais aliona namna ambavyo sehemu kubwa ya wake wa Marehemu walivyotengwa na kutambulishwa mke mmoja tu . Rais akaweka Sawa kumbukumbu na kusisitiza Marehemu alikuwa na wake zaidi ya waliotajwa.
Mifano ni Mingi Mingi Mingi mno.

Leo inasambaa Video na taarifa inayoonyesha mgogoro wa kujitakia kabisa.
Mgogoro ambao Rais kila Mara amefanikiwa kuukwepa, Mgogoro wa Kuheshimu mchango wa mtu mwengine hata kama ni Mdogo.

Nimemuona Mbunge wa Arusha Mjini God bless Lema analalamika, analalamika Mkuu wa Mkoa wa Arusha kushindwa Kuheshimu mchango wake katika kufanikisha upatikanaji wa Mradi wa ujenzi wa Wodi ya wazazi mkoani humo.

Ukiiangalia vizuri ile video, unaweza kuwadharau wote wawili,
Unaweza kumdharau Lema analalamika kutokuwa recognized,
Lakini unaweza pia kumdharau Mkuu wa Mkoa kwa kushindwa kuona mchango wa kiongozi kijana mwenzake hata kama wanatofautiana itikadi.

Haingii akilini katika shughuli za kiserikali kuona viongozi wa mikoa na wilaya wa CCM na au vyama vingine wakiheshimiwa akadharauliwa Mbunge hata kama wa Upinzani.

Kulikuwa na shida gani kwa Gambo kumtaja Mbunge Lema hata kwa kuwepo kwake tu pale?,
Kulikuwa na ugumu gani kwa Lema kumsubiri Gambo Amalize ili athibitishe kuwa kuanzia mwanzo mpaka mwisho kuwa hakumtaja na amepotosha kama alivyodai? .

Nawaona pia vijana wakijadili swala hili katika msingi wa KI-UKAWA UKAWA na KI-CCM CCM,
hapana vijana wenzangu, hili ni zaidi ya vyama vyenu, hili ni jambo linalitutaka tutumie Busara zaidi kuliko Ushabiki.

Hakukuwa na haja ya kurumbana kwenye hili,
Hakukuwa na sababu ya kuonyeshana misuli, kwamba mimi ni Mbunge na Mimi ni Mkuu wa Mkoa.
Hakukuwa na haja ya viongozi wetu kuonyeshana tofauti zao hadharani, tena mbele ya wanaowaongoza na wafadhili wa Mradi huo.

Hakukuwa na sababu yoyote ya viongozi hawa kugombea Fito katika nyumba wanayoijenga wao wenyewe.
Ni Wakati Sasa wa wateule wa MAGUFULI kubadilika.
Too much is harmful.
Nawasilisha
Ndimi
Habib Mchange