Showing posts with label Gossip. Show all posts
Showing posts with label Gossip. Show all posts

Hawa Ndio Wasanii 3 Ambao Lulu Anawakubali Kwenye Bongo Fleva

Msanii mahiri wa filamu Bongo, Elizabeth Michael aka Lulu amewataja wasanii watatu anaowakubali kwenye muziki wa Bongo Fleva.

Muigizaji huyo alikuwa akijibu swali la mmoja wa mashabiki wake kwenye mtandao wa Twitter, lililokuwa linauliza “wasanii gani watatu anaowakubali kwenye Bongo Fleva?”

Lulu alijibu swali hilo kwa kuandika, “Beka, Maua Sama na Alikiba.”

Juma Nature: Kuna Watu Wanahonga Ili Ngoma Zangu Zisipigwe

Ukizungungumzia historia ya muziki wa Bongo Flava, haiwezi kukamilika bila kulitaja jina la mkongwe Juma Kassim Nature aliyewahi kutamba ngoma kama ‘Jinsi Kijana’, ‘Hili Game’ na zingine kibao.

Hatimaye mkongwe huyo amaibuka na kudai kuwa kuna watu wanahonga ili nyimbo zake na za TMK Halisi zisichezwe redioni.

Nature amesema kuwa miongoni mwa watu hao ni uongozi wake wa zamani lakini hakuwa tayari kuwataja kwa majina.

“Sasa hivi kuna urasimu, kuna watu wanaenda kuhonga nyimbo zangu zisipigwe za Halisi zisipigwe, wapo watu wanafanya issue kama hizo na tayari tumeshaingia in deep kujua nini tatizo kwanini nyimbo hazichezwi,” ameniambia Nature nilipozungungumza naye nyumbani kwake Temeke.

Ikumbukwe Nature alikuwa akifanya kazi chini ya kundi la Wanaume Family kundi linalomilikiwa na Said Fella kabla ya kujitoa kwenye kundi na baadhi ya wasanii wengine waliokuwa kwenye kundi hilo na kuanzisha kundi lao jipya linalofahamika kama Wanaume Halisi.

Feza Kessy Anahisi Nando Anadata ‘Atafutwe na Asaidiwe’

Staa aliyewahi kuiwakilisha Tanzania katika shindano la Big Brother Africa, Feza Kessy, amesema kuwa anaamini Nando aliyewahi kushiriki naye kwenye shindano hilo, amepatwa na tatizo au anaugua kwakuwa tabia anazozionyesha zinampa mashaka.

Akiongea kwenye kipindi cha Kubamba kupitia Times FM, Feza amesema anaona akili ya Nando kama imevurugika kwa sasa. Anasema amekuwa tofauti na Nando, yule kijana mwenye nidhamu na mpole aliyekuwa akimfahamu.

“Naamini Nando ana tatizo asaidiwe,” alisema Feza. “Sijui kwanini lakini naamini Nando ana something hayupo sawa, sio yule Nando ninayemfahamu, naomba atafutwe asaidiwe,” alisisitiza.

Feza ambaye kwa sasa ni mtangazaji wa Choice FM, amedai kuwa aliwahi kukutana na Nando na akampa noti ya shilingi elfu 10. Anasema badala yake yake staa huyo aliitupa chini kwa madai kuwa haiwezi kumsaidia kitu.

Wema Sepetu a.k.a Tanzania Sweatheart Kuolewa Hivi Karibuni

Kwa taarifa nilizozinyaka hivi karibuni hukooo Instagram ni kuwa kipenzi cha wengi ( najua wengi mtabisha) si mwingine mrembo wetu Miss TZ 2006 na CEO wa kampuni ya ENDLESS FAME the one & only WEMA ABRAHAM ISAC SEPETU anaolewa hivi karibuni na model anaekuja kwa spidi ya 4G CALISAH ABDULHAMID.

Though hawaja comfirm wenyewe kuhusiana na habari hii ila nimejiongeza tu mwenyewe baada ya kuzinyaka picha hizi...

Video: Msami ameeleza sababu za kuachana na Irene Uwoya

Mtu wangu kama wewe utakuwa ni mpenzi wa kufuatilia mahusiano ya mastaa basi penzi la Mrembo kutoka Bongomovie (Irene Uwoya) na Mkali kutoka Bongoflevani (Msami)  litakuwa sio penzi geni kwenye macho yako leo  October 19 2016 Msami ameweka wazi sababu za kuachana na Ireen Uwoya
‘kuachana kama kuachana mimi sioni kama tumeacha kwasababu mimi na Ireen bado tunawasiliana sema tu mimi niliona kuna vitu haviendi sawa nikaamua kukaa pembeni yaani sina sababu maalumu ila niliamua tu mwenyewe‘>>>Irene Uwoya

Beny Kinyaiya Afungukia Ishu Ya Ushoga, Awaanika Wanaye

From Global
Mtu Kati: Vipi katika kupigapiga ‘gemu za nje’, umewahi kupata mtoto au watoto?

Kinyaiya: Yaah! Nina watoto wawili, wa kwanza anaitwa Ben Kinyaiya Junior, ana miaka minne na nusu na wa pili anaitwa Nilla, huyu ni wa kike na ana miaka mitatu.

Mtu kati: Kwa muda mrefu kumekuwa na madai ambayo hayajathibitishwa kwamba unajihusisha na mapenzi ya jinsia moja (ushoga), unalizungumziaje hili?

Kinyaiya: Ni mawazo yao tu, kwanza nikwambie mimi huwa siabudu majungu. Watu walianza kunizungumzia vibaya kitambo wakinihusisha na hayo mambo, wengine wakawa wanasema eti hawajawahi kuniona na mwanamke, nikawapuuzia tu. Baadaye kibao kikageuka, wakaanza kuniita eti mimi ni malaya kwa sababu nina wanawake wengi, pia sikuwajali. Nikaendelea na maisha yangu na sasa hivi ndiyo kama hivyo tena, tayari nina watoto wawili, waliokuwa wakinizushia mambo mabaya wote wamenyamaza kimya.

Mi nafanya shughuli zangu za kimaendeleo, sina haja ya kujibizana na watu wanaozusha maneno ya uongo juu yangu, kama mtu anahisi mimi nina matatizo yoyote basi aniunganishe na dada yake atampa majibu (anacheka).

Flora Mvungi Kaitaja Kashfa Ambayo Hatoisahau Maishani Mwake…

Ni headlines za msanii Flora Mvungi ambae leo October 19,  2016 amefunguka na kutaja kashfa ambayo hatoweza kuisahau maisha mwake.
Mimi sio mgeni macho mwa watu na wengi wananifahamu tabia yangu ikoje na wengi wanafahamu page yangu ya instagram ikoje na sijawahi kumtukana mtu bila sababu ya msingi kitu kikubwa’
‘Kikubwa ni kwamba ilivyotokea taarifa kwamba mimi ndio mmiliki wa ukurasa wa instagram uitwao Marashi ya pemba iliniumiza sana na kuniharibia hata kwa watu wengi ninaowaheshimu kwahiyo ningekupenda kuwaambia mashabiki wangu kwamba zile taarifa za mimi kumiliki huo ukurasa sio za kweli’

Wema Sepetu, Jackline Wolper, Bosi wa GSM ndani ya China kunani?

Kwenye Instagram zao mastaa hao wamepost waki safiri toka dar siku moja na wote wamepost picha wakiwa dubai same day then wote wamepost wakiwa china same place Canton Kama Picha zinavyoonesha Location ila hawajapiga picha pamoja.. Ambapo mdogo wa GSM counselor Salaah amepost akiwa Canton fair na wema na wolper wakipost wakiwa canton railway station same area ila wamekuwa makini kutopiga picha pamoja au labda hawafahamiani. Au labda ma baby wao idriss na harmonize ndo wamegharamia safari yao ya china.. Au labda yule MCM aliyempost kawasponso

Mr Bond Amjibu Auntylulu ' Nilipokuwa na Wewe Ulinikondosha Kwa Kero Nikawa Kama Mbuzi"

Bond Amjibu Auntylulu kupitia Ukurasa wake wa Instagram, Ameandika haya hapa chini baada ya Aunty Lulu Kudai alimuokota jalalani, kumlea na kumtafutia kazi ya kufanya Dar es Salaam..
____
From bond_bin_sinnan 
"Dah hii dunia hii jamani, Huyu nae sijui anamuda mrefu hajatoka kwenye magazeti?
Eti Leo anafufuka na kumtukana mke Wangu eti ameniiba mimi..
Hahahaha we Lulu wewe hebu muogope mungu wako wewe. Hivi una muda gani hata sura yangu hujawahi kuiona ? Zaidi ya miaka minne hata kuniona hujawahi Leo unaanza kuleta shida kwa mke Wangu.
We siunapenda umalaya na pombe sasa zimekukifu eti ndo unaamka usingizini? Basi kama umeamka Leo fahamu tulishaachana kitambo sana na Nina mke Wangu nampenda sana anaitwa Wastara
Naomba umuache ale raha kwa uwezo wake we subiri Global wakupe kiki upate mabwana wapya.
Nilipokuwa na wewe ulinikondosha kwa kero nikawa kama mbuzi wa sadaka mpaka kuku walinikimbia. Leo mtoto wa kiarabu ananisinga nang'ara navutia mpaka unanitamani tena unifuje. Hebu niache nipumue
Maskini sijui ndo uzee unakusumbua hahahaha.. Uwiii aleyo bhagosha lelaha le pogopogo lya bhose nzogi mlyee" Ameandika Mr Bond
Mr Bond na Mpenzi wake Mpya Wastara Juma

Lulu Diva, Amber Lulu Hakuna Bifu

Muuza sura kwenye video za Kibongo, Lulu Abass ‘Lulu Diva’ (pichani juu) na mwenzake Amber Lulu (pichani chini) hawana bifu lolote isipokuwa kuna watu wana mpango wa kuwagom-banisha.

Akichonga na Risasi Vibes, Lulu Diva alifunguka kuwa awali aliposikia kuwa Amber alimpaka matope kwenye ‘interview’ aliyofanya na redio fulani Bongo, alipaniki na kumtafuta ili amueleze kulikoni, lakini Amber alimwambia hakuna kitu kama hicho na kumtaka kuchunguza mwenyewe.

“Nilichunguza na kukuta kumbe si kweli, niligundua ni watu wasiopenda ushoga wetu ndiyo walikuwa wanajaribu kutukosanisha na si vinginevyo,” alisema Lulu Diva.

Aunty Lulu Awachana Mr Bond na Wastara...Adai Alimuokota Mr Bond Jalalani na Kumlea

Bifu Jipya mjini.....Aliyekuwa mpenzi wa zamani wa Mr Bond Aunty Lulu ameibuka pasipo julikana na kuanza kuwashambulia kwa maneno Mr Bond na Mpenzi wake Wastara...

Ameandika haya kwenye ukurasa wake wa Instagram:

Auntylulukimwana
"Nilikuokota jalalani mbwa wewe hujui hata kuvaa..ulikuja kwangu umevaa suruali kama alusi mabele au kanda bongoman wa zamani..ukaishi kwangu hata kazi huna mbwa wewe nikakutafutia mwenyewe channel 10..tena nikakuasa usije kuniacha..maana wakikuona watakutaka ukasema hatuwez kuachana...umepata kazi kwa mgongo wangu mwenzangu ukadindisha na kuwapa mti baadhi ya mastar(siwataji japo nawajua)na huyo ngedere wako kwa ujane akaamua kuwa wako..kumbuka mm ndo nilikupa taarifa ya kifo cha mumewe,,,alfajiri tumepata taarifa tulikuwa tumelala..we si ndo uliniomba turudiane ulivyoachwa akaenda kwa mbunge?nilikataa kwa kuwa nna mtu tayari!!leo hii kakurudia..utaishia hvyohvyo kukimbiwa ngoja atokee mkubwa zaidi ya mbunge yakukute..na usirudi hapa" Amendika Aunty Lulu

Kama ni Rahisi Kununua Tuzo, Wanaosema Hivyo na Wao Wakanunue – Babutale

Babutale amezijibu shutuma za baadhi ya mashabiki nchini kuwa wasanii wa WCB wamekuwa wakinunua tuzo.

Akiongea na Prince Ramalove wa Kings FM, Tale alikuwa na maneno mafupi tu kuwajibu. “Kama ni rahisi na wao wakanunue,” alisema meneja huyo.

Jumamosi iliyopita Diamond na Harmonize walishinda tuzo za Afrimma zilizofanyika jijini Dallas, Marekani.

Alidai kuwa tuzo hizo ni za Tanzania nzima na imeonesha jinsi gani mashabiki wako nao pamoja. Amesisitiza kwa kuwaomba waendelee kuwapigia kura wasanii wote waliotajwa kwenye tuzo za MTV MAMA wakiwemo wasanii wake wa WCB, Diamond na Raymond.

Wengine ni Alikiba, Navy Kenzo, Yamoto Band na Vanessa Mdee.

Q Chief afunguka jinsi Mtoto wake alivyo mfanya aogope kuendelea na matumizi ya madawa ya kulevya

 
Q Chief

Ikiwa ni mwaka mmoja toka msanii wa muziki, Q Chief akiri kutumia Madawa ya kulevya na kuamua kuacha mwenyewe, muimbaji huyo bado anaumia akikumbuka jinsi Madawa ya kulevya yalivyomwaribia maisha yake.

Muimbaji huyo ambaye mpaka sasa bado ana mashabiki wengi katika muziki wake, aliacha matumizi ya Madawa ya kulevya baada ya bintie kumuelezea adha anayopata shuleni.

“Nilijiuliza kwa nini namtesa mwanangu kwa kitu kisicho na faida, nikala kiapo kuachana na ‘unga’ na ninashukuru kwa sasa nimezaliwa upya, japo kila nikikumbuka namna nilivyotaka kupoteza nakosa amani,” Q Chief aliliambia gazeti la Mwanaspoti.

Kwa sasa muimbaji huyo ambaye yupo chini QS Mhonda Entertainment anajipanga kuachia wimbo wake mpya ambao video yake ameshoot Afrika Kusini.

Nyumba Aliyosema Barakah The Prince Anajenga ni ya Mama yake Naj, Kwa Mujibu wa Msanii Aliyeoa Kwa Akina Naj

Kwa wengi haikuwa rahisi kuamini maneno ya Barakah The Prince kuwa anamalizia kujenga mjengo wake aliouonesha kwenye Instagram.

Ni kwa sababu ujenzi si suala la lelemama na linaloweza kutokea kwa usiku mmoja. Pia wengi walitia shaka uwezo wa msanii huyo katika kipindi hiki kuweza kujenga nyumba kama hiyo. Na sasa huenda mashaka hayo yakawa yamepata uthibitisho wa uhakika.


Alawi Junior (katikati) akiwa na shemeji yake, Naj (kushoto) mwenye uhusiano na Barakah

Ni kutoka kwa Alawi Junior – msanii wa Bongo Flava aliyemuoa na kuzaa na dada yake Naj, Lady Naa. Alawi amepost Instagram video ya nyumba ambayo Barakah alidai ni ya kwake na kuandika: Done🏠👍Hongera sana Mama mkwe #zaharaDattan nyumba yako kali sana.”


Cha kufurahisha ni kuwa Barakah na mpenzi wake Naj Dattan walihojiwa na EATV na wote kuthibitisha kuwa ni nyumba ya Barakah!

“Namshukuru sana mke wangu Naj kwa sababu ana mchango mkubwa sana hadi hapa nilipofika pia kwa sasa siwezi kutaja fedha ambayo nimeitumia hapa kwa sababu ni hela nyingi sana hadi sasa na kama unavyoona nyumba bado haijaisha kwa hiyo nikimaliza kila kitu nitasema ni shilingi ngapi nimetumia,” Barakah The Prince alikiambia kipindi cha E-Newz cha EATV.

Swali ni kama maneno ya Alawi ni ya kweli, kwanini Barakah anadanganya?

Bongo5

Stan Bakora Ajibu Mapigo Kwa Barakah The Prince

Mchekeshaji maarufu Stan Bakora amefunguka juu ya povu lililomtoka Barakah The Prince siku kadhaa baada ya kuachia parody ya wimbo ‘Nisamehe’.

Kupitia kipindi cha Friday Night Live cha EATV, Stan amesema kuwa kama asingefanya vile video ingekuwa ya kawaida tu na isingeleta maana.

Barakah ameshindwa kuelewa. Kama nisingefanya vile ile video isingeleta maana, lazima uonyeshe uhalisia. Kwani Baraka si mweusi kweli?,” amesema Stan. Stan aliendelea kwa kumtania Barakah kwa kumwambia kuwa hapa mjini [Dar es Salaam] ndio kwanza ana Christmas mbili.

Awali baada ya Stan kuachia parody hiyo, Barakah aliandika kwenye Instagram: Matani ni mazuri ila yakizidi yanaweza kuleta matatizo… heshima ichukue nafasi yake tafadhali mzee utani huu sijaupenda iwe mwanzo na mwisho tafadhali.”

Mwimbaji Koffi Olomide Achukua Dakika Moja Kuwaomba Msamaha Wakenya Kwa Kumpiga Mwanamke

Mwanamuziki wa Congo Koffi Olomide ambaye mwezi July aliwasili  Nairobi Kenya  akiwa na wanamuziki wake pamoja na dancers wake kwa ajili ya show na baadae kuripotiwa kukamatwa kwa tuhuma za kumshambulia dancer wake wa kike ni baada ya kusambaa kwa video iliyomuonyesha akifanya kitendo hicho.

Koffi Olomide aliachiwa huru baada ya kutumikia kifungo cha siku mbili kati ya miezi 18 aliyohukumiwa awali,  na hiyo ilielezwa kuwa kuachiwa kwa koffi Olomide kulikuja baada ya Mahakama ya Kinshasa kusema kuwa hawakuona sababu za kutosha za kuhukumiwa kwa Koffi Olomide kutokana na tukio alilofanya JKIA.

Baada ya kupita miezi kadhaa tangu kutokea kwa tukio hilo na Koffi Olomide kutowahi kujitokeza hadharani kulizungumzia, amejitokeza kupitia kipindi cha Television cha Churchill Show amewaomba msamaha wakenya na mashabiki wake kwa ujumla na kusema …….

’Kupitia Churchill show, nataka kusema na nyinyi na kutuma ujumbe wa upendo, heshima na urafiki, mimi nasikitika kwa kile kilichotokea na maombi yangu nisamehewe kwa kile kilichotokea, mimi ni mwanadamu tu licha kwa kuwa ni maarufu’:- Koffi Olomide

Nataka Kuwa Mcha Mungu, Maisha ya Kuendekeza Dunia Nimeyachoka – Shamsa Ford

Malkia wa filamu na mama wa mtoto mmoja, Shamsa Ford amefunguka kwa kusema kuwa kwa sasa anataka kujikita zaidi kwenye ibada ya kufanya mambo ambayo yanampendeza mwenyezi Mungu.
Shamsa akizungumza baada ya kufunga ndoa

Mwigizaji huyo ametangaza uwamuzi huyo ikiwa ni miezi michache toka afunge ndoa na mfanyabishara wa maduka ya nguo, Chidi Mapenzi.

Maisha ya kuendekeza dunia nimeyachoka. Natamani ifike siku kwa kudra za Mwenyezi Mungu nibadilike. Natamani niwe mmoja ya wale watakaopata nafasi ya kwenda peponi pamoja na familia yangu . natamani nifanye IBADA kama ulivyoamua Mwenyezi Mungu. NATAMANI matendo yangu yawe ya kukufurahisha wewe Mwenyezi Mungu ili umauti utaponikuta niwe msafi..G9T MY PEOPLE. ..INSHAAALLAH MWENYEZI MUNGU ATUPE MWISHO MWEMA. .
Mashabiki wake katika mitandao ya kijamii wameonyesha kupendezwa na uwamuzi huo huku wachache wakimuuliza maswali kama ataendelea kufanya tena filamu.

Ruby Ampoza Vanessa Mdee Kwa Maneno Haya Baada ya Kukosa Tuzo

Ruby amemwandikia ujumbe wa kumsifia na kumtia moyo Vanessa Mdee baada ya kukosa tuzo ya Afrimma 2016 zilizofanyika wikiendi hii huko Dallas, Marekani.

Muimbaji huyo mwenye sauti ya dhahabu kupitia mtandao wake wa Instagram ameandika:

Tuzo aliyokupa Mungu love inatosha don’t worry about what happened yesterday ur still the best vee let them take that award this year but doesn’t mean that ur not the best 😫😫minnachojua tuzo yetu Tanzania tuendelee tu kufanya kazi kwaajili ya nchi yetu thats enough I know they know thats ur the one from TANZANIA....all in all love you @vanessamdee

Hata hivyo Vanessa hajaonesha donge lolote kwa msanii wa Kenya, Akothee aliyeshinda tuzo hiyo baada ya kupost picha yake na kumpongeza. Pia Jumapili hii alimpeleka lunch. Akothee alipost video akiwa na Vanessa na kuandika: Goofing around @vanessamdee yooo that lunch was hilarious thanks mamaaa 💪❤😍 but what lipstick has put together let not hand wipe.”

Pia alirepost picha aliyoweka Vanessa na kuandika: Kazi iendelee
Thanks mummy spending time with you at lunch was a great time spent.”

Diamond Platnumz, Harmonize na DJ D-Ommy ndio washiriki kutoka Tanzania waliofanikiwa kushinda tuzo hizo huku Linah, Alikiba, Yamoto Band na Mose Iyobo wakiwa ni washiriki wengine kutoka Tanzania waliokuwa wametajwa kwenye tuzo hizo.

NORA: Niliingia Vitani na Johari, Kisa Mapenzi!

KUTOKA moyoni! Bila kumtaja mwanaume husika, mwigizaji wa kitambo Bongo, Nuru Nassoro ‘Nora’amekiri kuwahi kuingia vitani na staa mwenzake, Blandina Chagula ‘Johari’ kisa kikiwa ni kugombeapenzi la mwanaume mmoja maarufu jijini Dar (jina ni siri yake).

Katika mahojiano maalum na gazeti hili, Nora alifunguka kuwa hali hiyo ilitokana na maisha ya usichana yaliyochangiwa na umaarufu na umri.

“Huyo mwanaume alikuja kwa lengo la kunitaka lakini nikawa nahisi kama Johari na baadhi ya rafiki zake walitaka kuninyang’anya, nikaamua kumvaa Johari,” alisema Nora ambaye kwa muda mrefu alikuwa haivi na Johari.

Ex wa Moses Iyobo Amgusa Kunako Aunty Ezekiel...Aunty Atoa Povu Hili....

Ex wa mcheza Dance Maarufu Moses Iyobo leo amepost picha ya Harmonize na Wolper akimpa Harmonize hongera kwa kushinda tuzo ya Afrimma, ndani ya ujumbe huo inaonekana kuna dongo kwa Mpenzi wa Moses Iyobo wa sasa Aunty Ezekiel...

Anty Ezekiel aliamua kujibu mapigo hivi:

Auntyezekiel
"Baby Cjui Ulimpa Nn yule jaman Mana anazunguka wee Anatoa tako koteee Ila hakusahau jaman Kumbe hata aliporudi back alikuwa mawindoni kashindwa kaanza Upya looh!Mlikuwa wote hata Mombasa hawakukujua maskini leo Hadi Afrima wanakutambua kumbe alikuwa anafatilia maskini bado ndio kwanza tunaanza safari...Ma lv mdogo mdogo ndio mwendo Achana na maneno yake alikuacha kwenye Geto wiki na miezi yy busy na Mganga leo ndio anaona wamaana au unaona watu hawaongei ww Binti plz just leave ma family Mama katafute na ww pakunyakua ukipata viwembe tena vumilia mwisho utapata wako ni Kupambana tuu Huyu si wako tena alichoka kukaa geto ma lv Pesa zote Unakula hata kupanga chumba kimoja kilikushinda hiyo Family au Mfano Hebu kataftie mtoto Baba acha kushindana na Mm am not ur type ma lv ... an huyu kurudi huko sahau boo boo an Ni mwanzo na mwisho kupost kuhusu ww nahisi Followers nilokupa wanakutosha.byee Enjoy ur life😘 #hutakiwikufanyahasira unatakiwa kukakaamaa kwani Ujenzi wa bila kazi Umemaliza#povulangulamwisho byeee" aliandika Aunty Ezekiel Kwenye Ukurasa wake wa Instagram