DAR ES SALAAM: Zikiwa zimesalia takriban siku 53 kufika Novemba 8, mwaka huu, siku ya Uchaguzi wa Urais wa Marekani, picha za mmoja wa wagombea wake kutoka Chama Cha Republican, Donald Trump na mwanamitindo wa kimataifa wa Tanzania, Flaviana Matata zinazowaonesha ‘live’ kwenye redcarpet zimeibua mambo, Ijumaa linafunguka.
DONALD NA FLAVIANA
Donald Trump ni mgombea urais tajiri ambaye ni mfanyabiashara aliyefanikiwa duniani na mwenye kauli tata dhidi ya wageni na matajiri wenzake nchini Marekani huku Flaviana Matata akiwa ni binti wa Kitanzania aliyetwaa Taji la Miss Universe Tanzania 2007. Akiwa mmoja wa mamodo wa kimataifa wenye mafanikio Bongo, Flaviana ambaye ni Mkurugenzi wa Flaviana Matata Foundation (FMF) kwa sasa anaishi na kufanyia kazi zake za kutangaza mavazi huko New York nchini Marekani, akiwa amepitia lebo nyingi kubwa za mavazi za nchini humo.
Donald Trump akimbusu Miss Albania 2010, Angela Martini na Flaviana Matata akishangaa.
ATANGAZA NIA, PICHA ZAIBUA MAMBO
Mara baada ya Donald Trump kutangaza nia ya kugombea nafasi hiyo, hata kabla ya kupitishwa na chama chake dhidi ya mgombea wa Democratic, H i l l a r y C l i n t o n n d i p o picha hizo zikaibuliwa z i k i w a na mjadala kabambe kwenye mitandao ya kijamii.
“Halohaloo… Ndiyo hivyo Flvav (Flaviana Matata) yupo na Donald Trump, Wabongo hoyeee… “Naona Flaviana yuko na shemela (shemeji) yetu mwenye CV na utajiri mkubwa duniani tena mgombea urais wa Marekani! “Ninavyojua mimi Flaviana ni mke wa mtu na aliolewa hivi karibuni ‘so’ hilo tukio na Trump lilikuwa kabla hajaolewa. “Nina uhakika huyo jamaa akishinda, Flaviana atakuwa ameulaa maana ni kiasi cha kumtumia tu picha zake na kumkumbusha walipokutana,” zilisomeka baadhi ya ‘komenti’ za wachangiaji wa picha hizo kwenye mitandao ya kijamii.
Trump akiwa na Flaviana Matata.
IJUMAA LATAFUTA UKWELI WA PICHA
K u f u a t i a m j a d a l a huo, Ijumaa lilizama na kuchimba ili kutafuta ukweli wa picha hizo a m b a p o l i l i b a i n i kuwa zilipigwa siku za nyuma huko New York, Marekani katika hafla ya kumpongeza mshindi aliyekuwa Miss Universe, Fadil Berisha.
Wakiwa katika pozi.
NDOA YA FLAVIANA
Flaviana ambaye ana mafanikio makubwa kupitia ulimbwende kiasi cha kuwa ‘role model’ wa mabinti wengi Bongo, alifunga ndoa na Deogratius Massawe Agosti 15, 2015 katika Kanisa la Mtakatifu Joseph na kufuatiwa na sherehe iliyofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar.
0 comments:
Post a Comment