Mwenyekiti
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, amesema
ataiburuza Serikaliya Awamu ya Tano mahakamani ili chombo hicho cha haki
kitoe tafsiri ya vitendo vya ukandamizaji wa demokrasia vinavyofanywa
na viongozi wa Serikali hasa Mkoani Arusha.
Mbowe
ameyasema hayo alipokuwa akilaani kitendo cha Mkuu wa Wilaya ya
Arumeru, kuwasweka selo madiwani wanne wa chama hicho akisema kuwa hiyo
ni ishara ya kwamba utawala wa awamu ya tano hauheshimu sheria.
“Nimewaagiza wanasheria wangu kwenda mahakamani ili kupata tafsiri sahihi kuhusu vitendo hivyo,” amesema.
Ameongeza
kuwa viongozi hao wamekuwa wakifanya vitendo vya udhalilishaji kwa
baadhi ya wabunge, madiwani, mameya na wenyeviti wa halmashauri kinyume
na sheria.
“Nawashangaa
sana Wakuu wa Mikoa na Wilaya wamekuwa wakiwadhalilisha wawakilishi wa
wananchi ilhali wao wakiwa ni waajiriwa ambao hawajaomba kura kwa
wananchi. Jambo hili limeanza mwaka huu, nah ii ni nafasi mbaya sana kwa
Rais Magufuli kuchagua makada badala ya watumishi,” amefunguka Mbowe.
0 comments:
Post a Comment