Beny Kinyaiya Afungukia Ishu Ya Ushoga, Awaanika Wanaye

From Global
Mtu Kati: Vipi katika kupigapiga ‘gemu za nje’, umewahi kupata mtoto au watoto?

Kinyaiya: Yaah! Nina watoto wawili, wa kwanza anaitwa Ben Kinyaiya Junior, ana miaka minne na nusu na wa pili anaitwa Nilla, huyu ni wa kike na ana miaka mitatu.

Mtu kati: Kwa muda mrefu kumekuwa na madai ambayo hayajathibitishwa kwamba unajihusisha na mapenzi ya jinsia moja (ushoga), unalizungumziaje hili?

Kinyaiya: Ni mawazo yao tu, kwanza nikwambie mimi huwa siabudu majungu. Watu walianza kunizungumzia vibaya kitambo wakinihusisha na hayo mambo, wengine wakawa wanasema eti hawajawahi kuniona na mwanamke, nikawapuuzia tu. Baadaye kibao kikageuka, wakaanza kuniita eti mimi ni malaya kwa sababu nina wanawake wengi, pia sikuwajali. Nikaendelea na maisha yangu na sasa hivi ndiyo kama hivyo tena, tayari nina watoto wawili, waliokuwa wakinizushia mambo mabaya wote wamenyamaza kimya.

Mi nafanya shughuli zangu za kimaendeleo, sina haja ya kujibizana na watu wanaozusha maneno ya uongo juu yangu, kama mtu anahisi mimi nina matatizo yoyote basi aniunganishe na dada yake atampa majibu (anacheka).

0 comments:

Post a Comment