VIDEO: Rais Magufuli kazitaja hujuma zilizokuwepo katika shirika la ATCL


Leo September 28 2016 Rais Magufuli amezindua ndege mpya mbili aina ya Bombardier Dash 8 Q400 zilizonunuliwa na Serikali kwa ajili ya kutumiwa na Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL). Uzinduzi wa ndege hizo za kisasa zilizotengenezwa nchini Canada, umefanyika katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Kabla ya kuzindua ndege hizo zenye uwezo wa kubeba abiria 76 kila moja, Rais Magufuli ameshuhudia makabidhiano ya mkataba wa ukodishaji wa ndege hizo kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi kwa niaba ya Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA) kwenda kwa Katibu Mkuu Uchukuzi Dkt. Leonard Chamriho kwa niaba ya Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL).

Taarifa ya ununuzi wa ndege hizo iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa ndege hizo ni mali ya Serikali na zitakodishwa kwa Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) kwa lengo kutoa huduma za usafiri wa anga ndani na nje ya nchi.

Ikiwa ni siku kadhaa zimepita tangua Rais Magufuli, amteue Mhandisi Ladislaus Ernest Matindi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL), leo wakati akizungumza kwenye uzinduzi wa ndege hizo Rais Magufuli ameeleza hujuma zilizokuwa zikifanyika kwenye shirika hilo…….

>>>’Shirika la ATCL halina mfumo wa kujiendesha kwa kujitegemea walikuwa wamezoea kutegemea fedha za serikali lilikuwa halijiendeshi kibisashara, walikuwa wamezoea mishahara inalipwa na Serikali, Shirika lilikuwa linajiendesha si kiueledi lilikuwa limebweteka, wafanyakazi wanafanya kazi kwa mazoea:-JPM

>>>’Viongozi na wakurugezi wa ATCL walikuwa wanajilipa 50000 kila wanapotembelea uwanja wa ndege wa Julius Nyrere wakikagua utendaji wa shirika, pamekuwepo na mtindo wa kugawana malipo ya ziada ya usafiri, wanagawana wao kwa wao na vituo vilivyokithiri kwa uozo ni pamoja na Comoro, Mwanza, Mtwara na Dar es salaam’:-JPM

0 comments:

Post a Comment