Baraka The Prince alisema haya kupitia kipindi cha Planet Bongo na kudai kuwa muziki anayofanya yeye ni wasanii wachache ambao wanafanya na kusema mara nyingi yeye anafanya jambo kutokana na mipango yake na matakwa ya mashabiki ila hafanyi kazi kwa kuangalia nani kafanya nini na nani.
"Siku zote mimi nasimama kama Baraka The Prince sijawahi kufanya kitu sababu fulani kafanya ila siku zote mimi huwa nafanya kazi kwa kuangalia mashabiki zangu wanataka nini na kuangalia mipango yangu. Kwanza sijawahi kufikiria kushindana na mtu yoyote yule kwenye muziki kwa sababu mimi najua nina muziki wa tofauti kabisa na miziki yao wanaofanya wao, watu wengi watafanya muziki wa mchaka mchaka watafanya nini lakini ukija upande wangu mimi watu tunaofanya muziki huu tunahesabika lakini kwenye miziki yao kuna watu karibia mia na kitu mpaka wengine hawajatoka wanafanya miziki yao" alisema Baraka The Prince
Mbali na hilo Baraka The Prince alisema kuwa yeye alikuwa na mipango ya kufanya kazi na Alikiba miaka mitano nyuma na anasema alijua kuwa wimbo wake wa sita lazima aimbe na Alikiba na imekuwa hivyo.
"Mimi nilikuwa na mipango ya kuja kufanya kazi na Alikiba miaka mitano nyuma na nilipanga kabisa wimbo wangu wa sita lazima niimbe na Alikina na imekuwa, mimi ni mtu ambaye huwa naishi kwa mipango saizi wimbo wangu wa kumi nishajua nitafanya na nani kama Mungu atazidi kutupa uhai, lakini pia ukiangalia muziki ninaofanya mimi na Alikiba ni sawa japo kuwa Alikiba yeye ni mtu wa kubadilika lakini nikisikiliza wimbo wowote wa Alikiba najifunza kitu hivyo yeye ni miongoni mwa wasanii walionivutia kwenye muziki huo wa Bongo Fleva" aliongeza Baraka The Prince
0 comments:
Post a Comment