Siku chache baada ya Waziri wa zamani wa Ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Muleba Kusini Profesa Anna Tibaijuka kushinda tuzo ya kimataifa ya “His Royal Highness Prince Khalifa bin Salman Al Khalifa Award for Sustainable Development” nchini Marekani na kuzikataa fedha zaidi ya milion 200 alizotakiwa kupewa kwa hofu ya kuhusishwa na zile tuhuma za Escrow
‘Kilichotokea
kwenye hii tuzo wanayosema nimekataa haina tofauti na pesa za
Rugemalila, sikukataa fedha hizo zaidi ya mil 200 bali sikuweza
kuzichukua kwasababu ya kisheria kwakuwa yangenikuta yaleyale ya Escrow‘ –Prof Anna Tibaijuka
‘Mimi
mwenyewe nimeziacha fedha hizo kwa masikitiko makubwa kwakuwa sheria
imenifunga, Sheria ya maadili ya nchi inasema kiongozi haruhusiwi
kuchukua zaidi ya elfu hamsini sasa ningezichukua kwangu ingekuwa
kizungumkuti‘ –Prof Anna Tibaijuka
‘Kwahiyo
mimi nikawaambia kule kwetu sheria ni ngumu kwahiyo nikawaambia hizi
fedha naziacha mezani kisha tukajipange na pia kama mnaweza itabidi hizi
fedha ziende zikawasaidie wananchi wa Tanzania kwenye matatizo yao‘ –Prof Anna Tibaijuka
Unaweza kuendelea kumsikiliza Profesa Tibaijuka kwenye hii video hapa chini…
0 comments:
Post a Comment