Video: Mabusu ya Ruby na Kijana Anayedaiwa Kuwa Mpenzi wake

Mkali wa wimbo ‘Na Yule’ Ruby ameshare video mbele ya mashabiki wake zaidi ya 260,000 katika mtandao wa instagram akibusiana na kijana anadaiwa kuwa ni mpenzi wake.

Muimbaji huyo alikuwa msiri kwenye mahusiano yake. Wiki hii amepost picha taofauti tofauti za kijana huyo huku akiandika ujumbe wa kimahaba hali ambayo imewafanya mashabiki wake kuhisi huwenda ni mpenzi wake.

Katika moja ya picha muimbaji huyo aliandika: Comedian wangu 👑 @_mantogoro love you baba 💋😘nyakunyaku stay away. Katika picha nyingine aliandika “My world” huku akimtag kijana huyo.

Muimbaji huyo kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake ‘Wale Wale’ aliouachia wiki chache zilizopita. Bongo5

0 comments:

Post a Comment