Utalipenda jibu la Martin Kadinda baada ya kuulizwa na shabiki kama Wema anatumia Madawa ya kulevya

Wiki hii kumekuwa na tetesi ambazo zinasambaa kwa kasi katika mitandao ya kijamii zikidai kwamba malkia wa filamu, Wema Sepetu anatumia Madawa ya kulevya ‘Unga’.

Tetesisi hiyo ambazo sio nzuri kwa mwigizaji huyo pamoja na watu wake wakaribu, zimeonyesha pia kuwagusa baadhi ya mashabiki wa mwigizaji huyo ambapo wanalazimika kutafuta ukweli wa tetesi hizo kwa namna yoyote.

Mmoja kati ya mashabiki wa malkia huyo kupitia mtandao wa instagram, aliamua kumuuliza meneja wa Wema Sepetu, Martin Kadinda kuhusu tuhuma hizo.

Pia rafiki wa karibu wa malkia huyo wa filamu aitwae Muna, kupitia mtandao wa Global Publisher amekanusha kumwingiza shosti wake Wema Sepetu kwenye matumizi ya Madawa ya kulevya kwa kusema madai hayo hayana ukweli.

0 comments:

Post a Comment