Mwanadada mrembo ambae amejipatia umaarufu mkubwa siku za karibuni kwa
kutokea katika videos kadhaa za Bongo Fleva Amber Lulu inasemekana
kwamba yuko chini ya usimamizi wa polisi kwa siku ya pili sasa.
Sababu ya kuwa chini ya Ulinzi inasemekana kuwa amekamatwa na Sembe
(Madawa ya kulevya) huko Airport mkoani Arusha akijiandaa kuyasafirisha
hadi nchini China.Gossip Cop Soudy brown alizinyaka taarifa hizo na
akaona haitakuwa mbaya kama atapiga story na watu wa karibu wa mwanadada
Amber Lulu ili kupata ukweli juu ya suala hilo.Ndipo alipomvutia waya
Gigy Money. Mapovu yaliyomtoka mwanadada Gigy sio ya polepole, na kudai
kuwa kimbelembele cha mwanadada Amber Lulu ndio kimemfanya kupata
matatizo.
Soudy Brown hakuishia kwa Gigy tu, alimvutia waya na rapper Young
Deeambaye kwa mujibu wa Gigy Money inasemekana kuwa ndiye boyfriend wa
mwanadada Amber Lulu. Na Young Dee alikana kabisa kumjua mrembo huyo na
akadai kuwa hajui chochote kinachoendelea kuhusiana na msichana huyo.
Ubuyu wote nimeukusanya hapa chini kwenye hii video unaweza kuitazama.
0 comments:
Post a Comment