Malaika afunguka haya ambayo yamekuwa yakimuumiza sana

 
Malaika

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Malaika ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake ‘Rarua’ amefunguka na kusema kuwa watu wanapokuwa wakitumia picha zake au wakiandika mambo yanayohusu maisha yake binafsi ni kitu ambacho kinamuumiza sana.

Malaika alisema hayo kupitia kipindi cha ‘Ngaz Kwa Ngaz’ kinachorushwa na EATV na kudai kuwa muda mwingine huwa anaudhika na kukasirika pindi anapoona watu wanachangia kwenye mitandao ya kijamii na kuhusisha mambo yake ya kimuziki pamoja na mambo yake ya kifamilia.

“Ninapokuwa napost picha kwenye mitandao ya jamii wakati mwingine napata ‘Comments’ mbalimbali nyingine zinakuwa zinaudhi, hasa pale mtu anapo kuja kuandika na kuhusisha maisha yangu ya muziki na maisha ya familia yangu ni kitu ambacho huwa kinaniumiza sana, na ni kitu ambacho sikipendi kwa sababu unapokuwa unanichukulia mimi kama msanii unatakiwa unichukulie mimi kama mimi. Na kama una jambo lolote unataka kuniambia niambie mimi kama mimi lakini huwezi ku ‘involve’ mambo yangu ya muziki na mambo yangu ya familia yanaumiza sana” alisema Malaika

0 comments:

Post a Comment