Linah Sanga
Msanii wa Bongo Fleva Linah Sanga maarufu kama ‘Ndege Mnana’ amefunguka na kusema kwa sasa hana ujauzito kama ambavyo watu wanahisi ila amedai kuwa yeye mwenyewe anatamani kuwa na mtoto na kusema muda si mrefu huenda mambo yakawa hivyo. Linah Sanga alisema hayo kupitia kipindi cha Friday Night Live ya EATV na kusema hivi sasa hana mimba ila soon mambo yanaweza kuwa hivyo kwani kwa sasa amejikita kufanya muziki na mambo ya msingi katika maisha yake.
“Hapana hii si mimba, nguo tu imesogea kwa mbele haya mambo huwa hayafichiki maana yataonekana tu, ila kiukweli soon mambo yanaweza kuwa hivyo. Maana saizi nimeamua kufanya muziki na mambo ya msingi, maana hata wazazi wetu wanafurahi kuona tukifanya mambo ya msingi kuliko mambo ya kijinga” alisema Linah Sanga.
0 comments:
Post a Comment