Faiza Ally
Msanii wa filamu Tanzania, Faiza Ally amefunguka kuhusiana na mwenendo wa tasnia ya Bongo Movie inayoendelea kwa sasa. Kupitia mtandao wa Instagram, muigizaji huyo amedai kuwa kwa sasa uigizaji si kazi ya kuichagua kuifanya labda uwe na njia mbadala tofauti na iliyopo sasa.
“Katika wasanii ambao wengi watakufa maskini Tanzania ni wasanii wa filamu… Na hii itakua Kama laana itakayo dumu kwa muda mrefu sana……! Wanaume wataishia kujenga labda na maisha ya kula Na kulala Na kulala na wanawake wengi huo ndio utakua utajiri wao ! Wanawake watalalwa wakizeeka wataachia wenzao itakua ndio mtindo …
Na ujana haudumu muda mrefu ! Mpaka pale ambao wanaume wataamua kufanya kazi Na kutenda haki Kwa wasanii hasa wa kike…. Na wanawake watakapo ona wana uwezo binafasi bila kutumia mastaa wa kiume kazini…. Na zaidi kutumia hela zao ktk kuwekeza ktk kazi …. kiukweli huwa nachoka sana pale ninapo ona haki hupati pamoja Na kufanya kazi … Kuna wkt najuta kuipenda sanaa… Na Ndio Maana Nilipo produce movie yangu ya kwanza niliacha Kwa muda mrefu sana …
Na nahisi baada ya hii mpya ntakaa Tena kuangalia soko Tena Kwa mara nyingine…. Kwa sasa filamu sio kazi ya kuchagua Na Kama unachagua Basi uwe Na namna ya kipato tofauti Na FILAMU…. Vinginevyo Kama mwanamke utaishia kugawa uroda mpaka yesu ashuke ! Kama mwanaume utabaki kuomba mpaka Basi…. Walio shika soko ni watu wenye roho mbaya ambao wanahisi wakiachia karakta zingine zitawashinda Na Kwa akili zao fupi wana hisi Ndio ujanja kumbe wana zidi kushusha soko la filamu….
Mm huwa namuona Diamond ni bonge la mjanja ambavyo Ana ibua wasanii wapya kupitia wasafi…. sio mjinga Kabisa amegundua hata kuwa Diamond milele….. yaani Kama ningekua nimejikita sana huko ningejambia hewani lkn MUNGU NI MWEMA kuna maisha zaidi ya filamu….. Any way lkn sitaacha kamwe kufanya filamu Kwa sababu napenda Lkn Kwa wkt Na sio kutumika kijanga….. Kinadada wanatumika sana lkn maendeleo hakuna Kabisa …. Wanaume wa bongo movie sio watu wazuri Kabisa …. Machoni Kama watu……“
0 comments:
Post a Comment