Sakata la Redio Kufungwa, Magic FM Yatakiwa Kuomba Radhi Siku Tatu Mfululizo, Redio 5 Yafungiwa Miezi

August 29 2016 Waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo Nape Nnauye alitangaza kuvifungia vituo viwili vya radio kwa muda usiojulikana ambavyo ni Magic Fm ya Dar es salaam na Radio 5 ya Arusha kwa makosa ya kutangaza na kutoa habari za kichochezi.

Waziri Nape alielekeza kamati ya maudhui kuviita vyombo hivyo na kuwasikiliza kwa kina kisha kushauri hatua zaidi ya kuchukua.

Leo September 16 2017 kamati imetoa maamuzi ambapo Magic FM wamepewa onyo kali na kutakiwa kuomba radhi kwa siku tatu mfululizo kuanzia kesho September 17 2016, Redio 5 imepewa adhabu ya kulipa shilingi milioni 5, kufungiwa miezi 3 na kuwekwa chini ya uangalizi wa mwaka mmoja.

0 comments:

Post a Comment