Mke wa Mtu Amponza Mwanamuziki Tunda Man

Msanii wa Tip Top Connection, Tunda Man ameshindwa kuachia video ya wimbo wake mpya ‘Mwanaume Suruali’ baada ya kumtumia mke wa mtu kama video queen.

Muimbaji huyo ambaye bado anafanya vizuri na wimbo ‘Mama Kijacho’, ameiambia Bongo5 kuwa ameshindwa kuachia kazi hiyo kutokana na mume wa mwanamke huyo kuzuia video hiyo sitoke.

“Kuna video ya wimbo wangu mpya ‘Mwanaume Suruali’ ambayo ilikuwa itoke hivi karibuni lakini kwa bahati mbaya mume wa video queen ambaye ametumika kwenye video amezuia video isitoke,” alisema Tunda. “Kwa hiyo bado tupo kwenye mazungumzo, kama akiruhusu itoke video itatoka hivi karibuni,”

Akifafanua zaidi kilichotokea Tunda alisema “Mimi nilikuwa nipo Dar nilimwachia mtu kazi Zanzibar ya kutafuta location na mambo mengine, kwa hiyo kwa bahati mbaya au nzuri akampata mwanamke ambaye na mimi nilipenda aonekane kwenye video. Kweli tukafanya naye video na pesa yake akalipwa, lakini mwanamke hakusema kama yeye ni mke wa mtu, kwa hiyo baada video kumalizika zile picha za behind the scene mume wake akaziona ndo akaamua kutushtaki ili video isitoke. Lakini tunashukuru mungu mambo yanaenda vizuri soon mambo yakienda kama yalivyopanga ngoma itatoka,”

0 comments:

Post a Comment