Miradi mikubwa 10 inayoendelea na inayotarijiwa kuanza hapa nchini

Leo September 14 2016 Gavana wa benki wa Benki kuu ya Tanzania Prof. Benno Ndulu ameitoa taarifa kuhusu hali ya uchumi nchini ambapo amezungumza mambo mbalimbali ikiwemo kutaja hii miradi mikubwa ya viwanda na miundombinu inayoendelea na inayotarijiwa kuanza kazi siku za usoni itakayochangia katika kuimarisha uchumi.
  1. Ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa (Standard gauge)
  2. Ujenzi wa bomba la mafuta la Uganda ambalo litahusu vile vile upanuzi wa bandari ya Tanga
  3. Ujenzi wa Export Processing Zone ya Kurasini – itakayokuwa mhimili wa biashara kati ya China na Ukanda huu wa Afrika
  4. Mradi wa kuzalisha megawati 240 za umeme wa Kinyerezi II unaoendelea kujengwa.
  5. Miradi ya kupanua viwanja vya ndege nchini kwa mfano- Dodoma, na mingine inayoendelea -katika viwanja vya Dar es Salaam, Mwanza, Mbeya n.k.
  6. Ujenzi wa maghala ya taifa ya kuhifadhi chakula yenye uwezo wa kuhifadhi tani 350 yatakayojengwa kwa msaada wa Serikali ya Hungary katika sehemu mbalimbali nchini hususan katika mikoa inayozalisha mazao ya nafaka kwa wingi.
  7. Kiwanda cha kuzalisha saruji cha Dangote kilichopo Mtwara ambacho kipo mbioni kuzalisha kulingana na uwezo wake (full capacity)
  8. Kiwanda cha kutengeneza marumaru cha Mkuranga, Pwani ambacho ujenzi wake unaendelea
  9. Kiwanda cha kuzalisha mbolea mkoani Lindi – kinajengwa
  10. Kiwanda cha bidhaa za chuma – mkoani Pwani ambacho kiko mbioni kukamilika.

0 comments:

Post a Comment