WIKI kadhaa tangu aingie katika uhusiano na jamaa
mmoja anayedaiwa kuwa ni kigogo, muuza nyago kwenye video za Kibongo,
Asha Salum ‘Kidoa’ kidogo anusurike kuachwa na kigogo huyo baada ya
kufumwa meseji za wanaume wengine kwenye simu yake.
Kwa mujibu wa chanzo kilicho karibu na muuza nyago huyo, tangu
ameanzisha uhusiano na kigogo huyo, ameonekana ni mtu mpole na hata
mambo ya starehe ameyaweka pembeni lakini kitendo cha kufumwa meseji
kimeharibu kila kitu:
![3](https://lh3.googleusercontent.com/blogger_img_proxy/AEn0k_vfu9Z6ryTwgh3eSySqCNCGS7sB7PfzYoUXB_QAw0kSKKN2fu5SUgsQejTzl-RRN_0MZRPq-d0h2y9ODg1TE4ISZ5TwA96BsINixaI_c8HvNNJ8wdDt_JFfGFpm8Jfj17f2Iboz=s0-d)
Kidoa
“Sasa unaambiwa juzi, Sikukuu ya Idd wakati yupo kwenye mtoko na
mpenzi wake huyo, muda wote Kidoa alikuwa bize akichati na mwanaume
mwingine jamaa akashtukia mchezo na kumpokonya simu, acha kinuke,”
kilisema chanzo.
Kidoa alipoulizwa na paparazi wetu alikana ishu hiyo kutokea ambapo alisema siku hiyo hakutoka nyumbani kwao.
0 comments:
Post a Comment