SIMBA
imejipanga kuhakikisha inaifunga Yanga leo na kuzidi kujikita kileleni
ambapo kocha wake Joseph Omog amesisitiza kuwa, kikosi chake cha sasa ni
cha ushindi na ndicho alichokuwa akikitafuta.
Kikosi
hicho cha Omog raia wa Cameroon kipo kileleni mwa Ligi Kuu Bara kikiwa
na pointi 16 katika mechi sita kikifuatiwa na Stand United yenye pointi
12 halafu Yanga inazo 10 tu katika mechi tano. Omog ambaye ameiongoza
Simba katika mechi sita na kushinda tano akitoka sare moja, alisema:
“Hii ndiyo Simba, tupo kamili kwa vita, Yanga naijua kuwa si timu ya
kuidharau lakini sisi tupo vizuri zaidi yao.
Mshambuliaji wa Simba, Mrundi, Laudit Mavugo.
“Wajiandae
na kipigo kwani tumedhamiria msimu huu kuwa mabingwa na kurejesha
heshima ya Simba iliyopotea kwa muda mrefu, nawaomba mashabiki waje
uwanjani kwa wingi kutuunga mkono.”
Omog
alisema ana imani kubwa na kikosi chake ambacho kiliweka kambi Morogoro
kwa siku nne kujiandaa na mchezo huo kabla ya kurejea Dar es Salaam juzi
wakati Yanga iliweka kambi Pemba hadi jana jioni. “Matokeo ya mechi
zangu za nyuma yananipa nguvu ya kushinda mechi hii, naomba wachezaji
wacheze katika viwango vyao tutafurahi,” alisema Omog.
Kikosi cha timu ya Simba.
AKIWAKOSA MAVUGO, AJIBU ANAWEKA
Kocha Msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja, amesema safu yao ya ushambuliaji ipo vizuri na akishindwa kufunga Laudit Mavugo basi Ibrahim Ajibu atafunga leo.
Kocha Msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja, amesema safu yao ya ushambuliaji ipo vizuri na akishindwa kufunga Laudit Mavugo basi Ibrahim Ajibu atafunga leo.
Wakishangilia kwa pamoja.
“Takwimu
zinaonyesha jinsi safu yetu ya ushambuliaji ilivyo imara kwa kufanikiwa
kufunga mabao mengi, tumejiandaa vizuri kupata mabao kwa Yanga na
wakijidanganya kumzuia Mavugo asifunge, Ajibu na wangine wapo na
wanaiweza kazi hiyo,” alisema Mayanja, raia wa Uganda.
Straika wa Simba, Mavugo akizungumzia mchezo wa leo, alisema: “Jumamosi (leo) ndiyo itakuwa hukumu ya Yanga kwa sababu nimejipanga kuwanyoosha na kuisaidia timu yangu kupata ushindi.”
1. Vincent Angban
2.Janvier Bukungu
3.Mohammed Hussein ‘Tshabalala’
4.Juuko Murshid
5.Method Mwanjale
6.Jonas Mkude
6.Jonas Mkude
7.Shiza Kichuya
8.Muzamiru Yassin
9.Laudit Mavugo
10. Ibrahim Ajib
11. Jamal Mnyate
AKIBA:
1.Manyika Peter 2.Hamad Juma 3.Mohammed Ibrahim 4. Mwinyi Kazimoto
5.Novart Lufunga 6.Said Ndemla 7.Frederick Blagnon Imeandaliwa na
Nicodemus Jonas, Sweetbert Lukonge, Said Ally na Omary Mdose.
0 comments:
Post a Comment