Matt Fiddes, aliyefanya kazi kama bodyguard wa MJ kwa miaka 10, anasema alishangazwa mno na majambazi waliopita kwenye mlango wa hoteli ya kifahari ya de Pourtalès alipokuwa anakaa Kim– achilia mbali kufika hadi chumbani kwake.
Kardashian alikuwa akilindwa na mlinzi wake mkuu, Pascal Duvier alipovamiwa na kutishiwa bunduki. Awali alikuwa na dada zake wawili walipokuwa wakijirusha kwenye klabu ya usiku.
Nyota huyo, 35, aliibiwa pete na mikufu ya thamani na watu hao waliokuwa na silaha, wakiwa na vinyago usoni na wakiwa wamevalia kama polisi.
Akizungumza na MailOnline, bodyguard huyo wa zamani na gwiji wa sanaa ya mapigano, alisema: Watu pekee wa kuwalaumu, ni timu yake ya ulinzi. Ni mwanamke maarufu zaidi duniani, huenda akawa anajulikana kumzidi hata rais wa Marekani.
“Ana mamilioni ya mashabiki na anatakiwa kuwa na walinzi waliojiandaa. Nilipokuwa na Michael hilo lisingetokea. Majambazi lazima wangepita kwenye mlango wa mbele, achilia mbali kwenda chumbani kwake,” alifafanua.
Akielezea jinsi alivyokuwa akifanya, alisema: Tungevikagua vyumba kabla hajaingia na kila muda alipoenda popote. Tungekuwa na watu mlangoni na mtu mwingine kwenye njia ya kwenda chumbani na hata kumwamsha kila baada ya saa tatu au nne kuangalia kama yuko sawa.”
“Yupo kwenye level sawa. Ni nyota mkubwa.”
Amedai kuwa shambulio jingine la mtu aliyemvamia hadharani Kim akitaka kumbusu makalio yake, lingekuwapa angalizo kubwa la kuweka mambo sawa.
Anadai kuwa Michael Jackson alikuwa na walinzi 50 hadi 60.
0 comments:
Post a Comment